Sunday, November 24, 2013

BLOGS ZINAVYO MKERA RAIS KIKWETE"TETEENI NCHI NA SI KUIPONDA KWENYE BLOGS"

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete ameonyesha kukerwa na tabia ya baadhi ya watanzania wanaotmia muda wao mwingine kwenye mitandao ya kijamii Blogs kuiponda nchi yao, Akizungumza na Watanzania waishio nchini Pland alisema kwamba, "Teteeni nchi badala ya kuiponda kwenye mablogu", Rais Kikwete amesema wajibu mkuu wa Watanzania wanaoishi nje ya nchi ni kuisemea vizuri, kuihangaikia na kuitetea nchi badala ya kushinda kwenye mablogu wakiiponda, kuibeza na kulalamika.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa kuishi kwa Watanzania nje ya nchi kutaonekana jambo la maana zaidi ikiwa watatumia rasilimali na fursa wanazozipata ugenini kusaidia kubadilisha hali na maisha ya ndugu zao waliobakia Tanzania. Rais Kikwete pia amewaonya Watanzania hao wasije kuchanganyikiwa na kujichanganya wenyewe kwa kuiga tamaduni za kigeni kupita kiasi. Rais Kikwete alikuwa anazungumza na Watanzania waishio nchini Poland usiku wa jana, Alhamisi, Novemba 21, 2013, kwenye Hoteli ya Bristol mjini Warsaw ambako alifikia wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku nne katika Poland.

Aliwaambia Watanzania hao na familia zao: “Matumaini na matarajio yetu sisi tuliobakia nyumbani ni kwamba mtaisemea vizuri nchi yetu, mtaitetea nchi yenu, mtaihangaikia nchi na kuleta faida nyumbani. Ni jambo haliingii akilini kuwa baadhi yenu mnaweza kuishi hapa na kazi yenu ikawa ni kushinda kwenye mablogu mkilaumu nchi yenu wenyewe. Nchi mbaya, viongozi hawafai..mnapata faida 

gani. Mnazo nchi ngapi?”Rais Jakaya Kikwete akitafakari jambo juu ya utawala wake

Aliongeza Rais Kikwete: “Kuhangaikia nchi yetu ni wajibu wenu ambao hamwezi kuukwepa. Matumaini yetu ni kwamba mtasukuma mbele maslahi ya nchi yenu, mtatetea ustawi wa nchi yenu na ndugu zenu.

Fursa zilizoko hapa mnazijua wenyewe, sisi hatuzijui. Nyie ndio mnaishi hapa, sisi tuko mbali na hatuwezi sisi kutegemewa na kutarajiwa tufanye mambo ya hapa ambayo hatuyajui.”

Alisisitiza Rais Kikwete: “Mbona kazi za ma-Ngo’s mnazifanya vizuri bila kusukumwa ama kushawishiwa lakini kazi za kusaidia ndugu zenu hamfanyi? Kama hata hamwezi kusaidia ndugu zenu mnachangia nini nchi yenu?.

” Rais amesema kuwa kwa Watanzania waishio nje kuonekana wanajali na kutetea nchi yao kutasaidia kujenga hoja ya msingi kuhusu umuhimu wa kuanzishwa kwa uraia pacha (dual citizenship) ambao Watanzania waishio nje wanaulilia. “Mnaweza kuhalalisha hoja ya uraia pacha kwa kuwa watu wenye faida kwa nchi.”

Kuhusu ombi lao la uraia pacha, Rais Kikwete amesema kuwa ni wajibu wa Watanzania waishio nje kuongeza kasi ya kuchangia mjadala kuhusu suala hilo ili likubaliwe kuingizwa kwenye Katiba Mpya. “Rasimu ya kwanza ya Katiba ililikataa jambo hilo kwa sababu hili ni jambo lisilokuwa na ushabiki na upenzi mwingi nyumbani.

"Ujumbe wangu kwenu ni jipangeni vizuri kutetea hoja yenu hii. Saidieni mjadala wa jambo hilo badala ya kushinda kwenye mablogu mkijadili siasa na hivyo kusahau yenye maslahi kwenu.”

Kuhusu kuiga tamaduni za nchi nyingine na kusahau za nyumbani, Rais Kikwete aliwaambia kuwa inaelekea kuwa baadhi wachache wanaoishi nje ya nchi, wamejichanganya na kuchanganyikiwa kiasi cha kusahau mambo ya kwao. 
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo baada ya mmoja wa Watanzania kudai kuwa suala zima la mahari limepitwa na wakati na kuwa kutoa mahari ni sawa ni kuwauza watoto wa kike. Rais ambaye alionyesha kushangazwa na kauli hiyo, alijibu: “Msiige mambo ya kigeni kiasi cha kuanza kuchanga

6 comments:

Anonymous said...

Tumesikia lakini bw.Rais hebu tuwekane sawa kidogo maanake tunapoishi huku ughaibuni tunajifunza mengi mojawapo ikiwa ni kutokuwa waoga na kuachana na siasa za kinafiki... Tutatetea pale kwenye ukweli na tutakosoa bila woga ,aibu wala unafiki! Serikali inapofungia magazeti na wanahabari wanapoteswa na kupoteza maisha kwa ajili ya kuandika ukweli tuwezi kutetea!! Kwanza ukiwa kama Rais unatakiwa kuelewa kuwa kukosolewa ni kuzuri.. Hivi tukiisifu serikali yako kweli watendaji wako watachapa kazi? Hii dhana ya kusifiwa hebu tuiache kwani imepitwa na wakati.. Bw.Rais unatembea sana na ni mtu smart tu..tuangalie ukweli na kuiga yenye maana tusipende sifa tusizostahili!! Tanzania inanuka kila sekta ...madawa ya kulevya, utendaji mmbovu na wizi wa Mali za umma uliokubuhu , tembo wetu wanateketea ,pesa zinaibwa na kufichwa Uswis ni baadhi tu ya madudu yanayoitambulisha Tanzania kimataifa! Sasa tudangaje? Mungu ibariki Tanzania .

Anonymous said...

hatuipondi nchi, tunawaponda nyinyi viongozi, samaki mmja akioza.....

Anonymous said...

Watanzania wanachukia uongozi wa nchi kwa kutowajibishana, Msingi mkubwa katika nchi ni kuwajibishana, likifanyika hilo kila mtu ataipenda nchi na viongozi.

Anonymous said...

Serikali ya Tanzania imeoza, waziri anabaka mtu, badala ya kuwajibishwa, anapelekwa Sweden, really?mijitu imejilimbikizia mipesa, dawa hospitali haluna,, matumbo makubwaaa kila umuona katika uongozi, tafadhali bwana Raisi, u have very smart people, especially those who no longer count themselves as Tanzanians, usianzishe hii mijadala itakutia aibu....

Anonymous said...

Nakuunga mkono Raisi si vyema kuiponda nchi ila ni busara sana kutafuta ufumbuzi wa matatizo kama yapo. Maa kuiponda hakujengi ila kunabomoa zaidi.

Anonymous said...

hatuna sababu ya kusifu nchi ili tupewe uria wa. nchi mbili.uraiya wa nchi mbili ni haki yetu ya kimsingi na tutaipata just the matter of time.watanzani waishio nje wakiwa tayari they will fight for it.haki haiyombwi.