ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 6, 2013

DIAMOND: SITUMII KINGA, NASAKA MTOTO!

Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz'.

HUWEZI kumkwepa Diamond katika ulimwengu wa habari! Staa huyo wa muziki wa Bongo Fleva ambaye jina alilopewa na wazazi wake ni Nasibu Abdul, ameibua mengine mapya, akidai hapendi kabisa kutumia kinga awapo faragha.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko kwa njia ya simu wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, Diamond katika maelezo yake, alionesha wazi suala la afya yake siyo ishu sana, muhimu kwake ni mtoto.
Penniel Mungilwa ‘Penny’.

KILIO CHA MTOTO
Diamond alisisitiza kwamba kwa sasa kiu yake kubwa ni kupata mtoto na siyo vinginevyo.
“Nashukuru maisha yanakwenda vizuri lakini nitakuwa mwenye furaha zaidi kama nitabahatika kupata mtoto. Mwanamke atakayenizalia, atakuwa amekamilisha furaha yangu,” alisema Diamond.

Staa huyo wa singo ya Number One inayosumbua kwenye chati mbalimbali za muziki, alisema siku akiitwa baba, atakuwa amefungua ukurasa mpya kabisa kwenye maisha yake.

“Ni furaha yangu kuitwa baba. Unajua huwa naangalia... kuna baadhi ya marafiki zangu tayari wamepata watoto. Hata Wasafi kuna madensa wangu wana watoto. Nahisi nami nikipata nitakuwa na amani zaidi,” alisema.
Wema Sepetu.

VIPI MAGONJWA?
Pamoja na kiu yake hiyo ya kupata mtoto, kutokutumia kinga kunamuweka mtu kwenye hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa hatari ukiwemo Ukimwi, kuhusu hilo Diamond alisema, hana wasiwasi, anajiamini.

“Kwanza mimi huwa napima Ukimwi mara kwa mara, nipo sawa. Najiamini kwa asilimia mia moja lakini pia siyo kiruka njia. Sina maana kwa sababu natafuta mtoto, basi kila mwanamke nakutana naye tu. Hapana.

“Mimi nawaamini wanawake wangu... isitoshe wanajulikana. Kifupi tunaaminiana na ninatafuta mtoto ndani ya hao, siyo vinginevyo,” alisema.

Jokate Mwegelo.

MTOTO NJE YA NDOA?
Kuzaa kabla na nje ya ndoa haikubaliki katika jamii yetu lakini pia hata imani anayoiamini Diamond inakataza, alipoulizwa alisema haoni tatizo, anataka mtoto.

“Kaka, kaka, kaka...mbona huelewi? Hayo yote nayajua lakini cha msingi hapa mimi nimesema nahangaikia mtoto na ninatamani sana kupata mtoto ambaye naamini atakamilisha furaha yangu,” alisema.
Rehema Fabian.

MAMA WA MTOTO ATAOLEWA?
Hata hivyo, Diamond alisema mwanamke atakayemzalia mtoto siyo lazima ndiye awe mke wake wa ndoa kwa sababu suala la ndoa ni jingine na kuzaa ni jingine.

“Wangapi wanazaa na wanaheshimiana bila kufunga ndoa? Suala la ndoa ni kubwa, siyo la kukurupukia. Inawezekana mwanamke akanizalia na akiwa na tabia ninazopenda akawa mke wangu lakini inawezekana tukaishia kuzaa tu.

“Kifupi suala la ndoa ni mipango. Ikiwa sawa basi nitaoa lakini kwa sasa ninachozungumzia ndugu yangu ni kupata mtoto, baaasi!” alisisitiza Diamond.

WALIOPITA KWA DIAMOND
Diamond amewahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na wasichana kadhaa, kati yao wengine walikubali na wengine walikana uhusiano huo huku baadhi mapenzi yakiwa ya siri.

Baadhi ya wasichana waliowahi kuwa penzini na Diamond ni pamoja na Jacqueline Wolper, Wema Sepetu, Rehema Fabian, Jokate Mwegelo, Pendo Mushi na Penniel Mungilwa ‘Penny’ ambaye mpaka sasa yuko mikononi mwake.

Wema wakati penzi lao likiwa motomoto, ilisemekana ana ujauzito lakini ghafla ikawa kimya, ilikuwaje? Diamond anafafanua: “Alisema ilitoka, sasa ningefanyaje? Lakini pia sipendi kuzungumzia sana mambo hayo yaliyopita. Tuongee kuhusu yajayo.”

Kuhusu mimba ya Penny? Huyu hapa Diamond: “Ni kweli aliwahi kusema kuwa ana mimba yangu lakini baadaye alisema imeharibika. Siwezi kusema zaidi ya hapo.”

KUTOKA RISASI
Kila mmoja ana uhuru wa kupanga na kuamua maisha aliyoyachagua. Wazo la kuwa na mtoto ni zuri lakini ni vyema Diamond akawa makini ili kiu yake hiyo isije ikazima ndoto zake katika maisha.

Suala la kuchunguzana afya kabla ya kuamua kukutana na patna bila kinga liwe dira kwake wakati akiwa kwenye harakati hizi za kutafuta mtoto. – Mhariri. GPL

7 comments:

Anonymous said...

Sasa huyo penny anang,ang,ania nn bwana ndo hana mpango wa kuoa wala fikri hanaaa uwiiii poleee

Anonymous said...

Nilikuwa sijui kama kuna watu wenye fikra ndogo kama huyu Diamond. ELIMU NI MUHIMU SANA HE NEEDS TO GO BACK TO SCHOOL, Mwanamme gani anayedream kumzalisha mwanamke bila kuongelea ndoa kwanza labda wewe PAGANI AU HUAMINI KAMA KUNA MUNGU! THIS STORY IS TRASH NA INAKUPUNGUZIA HESHIMA KATIKA JAMII. ANGALIA HATA MASUPER STAR WAKUBWA WENYE PESA ZAO JZ, MICHAEL JACKSON WALIOA KWANZA NDO WAKAZAA WATOTO. USIANZE ULIMBUKENI DINI YA KIISLAMU IPO WAZI SANA KWENYE SUALA HILI LA KUZAA NJE YA NDOA. DINI YETU INASISITIZA KUOA MAPEMA AT PUBERTY! YOU ARE TOO OLD TO TALK THIS NOSENSE, YOU BETTER CHECK FOR HIV AND HPV USIJE UA WATOTO WAWATU WAZURI NA MAGONJWA YA ZINAA.

Anonymous said...

jamaa bado hajatulia so msimlaumu jamani ujana bado unamuwaka moto na dini yake hata hajui ndo maana anaropoka ovyo mwenzenu yuko kwenye kuuza sura na magazeti shauri yenu asije akawa anakuchanganyeni kwa maneno yake huku mambo yake ya maisha anayajua yeye na anayapanga safiiiiii tulizeni munkar wenzangu mnaotuma comment mwenzenu mimi nimeshajifuza huwa tunasomaga sana kwenye ma blog na kuambiwa hivi na vile lakini kiukweli akili kichwani take care

Anonymous said...

Nasibu kidini haikuruhusu kupata mtoto n'nje yandoa,isitoshe wewe unataka mtoto umepima kama sperm zako zina nguvu ya kuzalisha?Usifikiri kuwa na nguvu ya kusex na kupez ndio kupata mtoto!Unaweza ukahangaika sana na wanawake wakila aina na mtoto usipate,Ushauri wa bure tafuta mwanamke ambaye unampenda nendeni mkacheck afya ya uzazi from there mplan kutafuta mtoto na kumtanguliza mungu mbele.Pesa unayo acha kukurupuka na kusema pumba better think before saying something.Acha mi sifaaaaaa sisi fans wako tunakutakia kila la heri.

Anonymous said...

Nasibu acha udakuzi, haya maneno hayako na sifa uliyo nayo, Swala la kupata mtoto linatakiwa kufanyiwa utaratibu na uelewano sio unavyojitemezea tu ukidhani atakayezaa,hivi ni nani atakayebeba huo mzigo bila ya makubaliano, usione ukiwadungua kila siku wanataka pesa yako tu. Hivi hao wote unaowapata unauhakika nao? Bila makubaliana na maelewano ya kimaisha nani yuko tayari kujipotezea muda wakati wewe ni donoa donoa!!

Anonymous said...

si uzae na dada zako ukoo usiende mbali. idioot

Anonymous said...

The way u r ugly unadhani ni rahisi hao warembo wakuzalie bila hata ya ndoa?ndo maana wanabeba mimba wakitarajia utawafariji kwa ndoa na wanapogundua haipo hakuu mwenzangu toto na domo kama la baba yake alafu hata kindoa cha kunistiri na kunifanya nisichekwe hakipo vimimba vinaharibika kwa stress. Tunajua pesa sometimes inaweza kukufanya upinge au ugeuze ya mungu lakini hata imani na mwanamke huna? na ndiye aliyekulea? inshallah mungu akuonjeshe hayo kwa dada zako, upate wapwa bila ndoa. stupid elimu dunia tunajua huna basi hata ya aghera unaipuuza eeh binadamu mwenzanguuu weee pumzi zisikudanganye!!!!!!!