ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 5, 2013

KAMA HAMTOFAUTIANI, MNADANGANYANA


KATIKA suala zima la uhusiano, yapo mambo mbalimbali ambayo tumekuwa tukielezana, lengo kubwa likiwa ni kuwekana sawa, ili kila mmoja wetu aweze kuhakikisha penzi lake linadumu na kuwa salama kwa muda wote.

Uhusiano una mambo mengi sana. Kila mmoja kati yetu angependa kuwa na uhusiano ulio bora na wenye kuweza kuwa mfano kwa wenzetu. Sidhani kama kuna mtu ambaye ni shabiki wa vurugu katika uhusiano.

Wakati hali iko hivyo, lipo jambo moja ambalo kwa makusudi tunakataa kulikubali, wakati ukweli ni kwamba ni la msingi na lenye kupaswa kuzingatiwa sana. Kama nilivyosema, hakuna mtu anayependa uhusiano wenye matatizo, kila mmoja angependa maisha yawe laini kwa kadiri inavyowezekana.

Lakini ni vyema wote kwa pamoja tukatambua kwamba uhusiano ambao hauna msuguano ni uhusiano wenye kutia shaka.
Kwa kawaida, mke ni lazima awe na wivu juu ya mumewe, sawa sawa na mume anavyotakiwa kuwa. Endapo utaona mume au mke wako hana matatizo na wewe, jua wazi kabisa kuwa unaibiwa.

Kuna watu wengine utawasikia wakisema “Ah, mke wangu miye bwana mzungu, hata nirudi nyumbani saa ngapi hana matatizo, siyo kama wengine wakichelewa kurudi kwao huwa shughuli.”

Ni jambo gumu na lisilowezekana mke wako asiwe na tatizo mumewe anapochelewa kurudi. Au vilevile kwa wanawake, wapo ambao hudai kuwa waume zao ni ‘wazungu’, kwamba hawana matatizo nao hata kama watachelewa kurudi toka makazini mwao.

Kwamba hata wakiwaona wanazungumza kwa vicheko na watu wengine wa jinsia tofauti, hawana wivu na wanaona poa tu.
“Mimi mke wangu hata aone nambusu mwanamke hapa, hana noma,” utawasikia baadhi ya watu wakitoa kauli kama hizi.

Ingawa ni kweli kuwa wapo baadhi ya wenzetu wenye uvumilivu mkubwa, lakini linapofika suala la mke au mume, ni vigumu kuamini kirahisi.

Hakuna mwanaume asiyekuwa na noma kwa mke wake na wala hakuna mke asiye na noma kwa mume wake. Kinachotokea katika nyakati kama hizi ni uongo wa kila mmoja. Kama kila mmoja anakuwa ni muongo, basi hujifanya kutokuwa na noma na mwenzake ili naye aachane naye.

Anajua kama hatafuatilia mambo ya mwenzake, basi uwezekano ni mkubwa na yeye kutofuatiliwa mambo yake.
Na inapotokea jambo kama hili ni wazi kuwa watu hawa hawapendani. Wanaishi pamoja kwa shinikizo maalum. Ndiyo, hili lipo, wapo watu wanaokuwa katika uhusiano lakini wakiwa hawapendani.

Wanalazimika kuishi hivyo labda kutokana na ugumu wa maisha, ndoa za lazima, shinikizo la wazazi na kadhalika. Ndiyo maana katika hali kama hiyo, hakuna anayemjali mwenzake kwa dhati.

Kama nilivyosema hapo awali, wapo watu ambao huweza kuvumilia kumuona mwenzake akivurunda. Ingawa jambo hili hufanyika, lakini ni lazima tuelewe kuwa wanaovumilia bila kupiga kelele huumia zaidi kuliko wale wanaong’aka na kufoka.

GPL

3 comments:

Anonymous said...

Nimefurahi sana kusoma makala hii na hasa hasa kichwa cha habari kimenivutia sana na hongera sana muandishi na dj luke kwa kuweka makala hii.
kwa kweli nimekubaliana na maandiko yako umesema kweli lakini pia tukubaliane kuna watu wa design hii ambao wako kama wazungu na wala hawadanganyanyi ni kweli wanapendana kikweli kabisa wanaheshimiyana ndo maana wanakuwa hawana pressure na mwenzake kwa sababu wanajua mwenzake anampenda na yeye anampenda tukubaliana jamai si wote wanaojifanya wana wivu wa mkee au mume ndo wanapendana kikweli au wana hisia kali si kweli sikubaliana nalo kuna wengine wanawapaka mafuta ya mgongo wa chupa wenzao kujidai kupendana sana kumbe wapi wanakula kwenginew na kuonyesha show kwamba nina wivu na mke wangu au mume wangu ili kuficha makucha yapo tena yapo sana haya jamani tusidanganyane eeti akiwa na wivu na mimi ndo ananipenda no and no kila kiumbe ameubwa tafauti ndo maana nikavutiwa sana na kichwa cha habari nilidhani ungeleta mambo kama haya ya utafauti because hatufanani tumetafautiana kinjisia, malezi nakazi kielimu kiuchumi kiutaifa na mengi mengi so tusiweke assumptio kwamba kama mtu haonyeshi wivu hanipendi wakati ndo mapenzi yangu haya ya kutokuwa na wivu lakini ukifuka mipaka nitakuja ku react na kuvunja mahusiano na utashangaa imekuwaje so tujaribu kuchambua mmabo jamani.

any way hongera sana kwa nakala nzuri

yule yule NY

Anonymous said...

maada nzuri sana hii na nikweli kuna wengi wanaoa au kuolewa kwa wanavyofikiria wao si wote huwa wapo katika ndoa wanapendana kweli ni wachache na ndo maana unaona matengano ni rahisi sana kutokea kwa sababu hakuna aliye na pendo la dhati na nikweli ni lazima kuonyeshana mnavyopendana na kawivu kadogo cha hapa na pale lakini si wivu wakupitiliza au kuwa gubuuu unamnyima mwezio amani ya kukupenda ndani ya moyo kikweli kweli lazima tukumbuke tumelelewa tafauti mazingira tafauti upeo wa kifikiria upo tafauti na maisha tunayaonaje kila mmoja ana akili zake cha muhimu tuheshimiyane na tuwe tunajaribu kuzikosoa tafauti zetu kwa kiungwana na kutumia hekima na busara na upendo wa hali ya juu siyo kubezana.

mapenzi si mchezo ni full time job usisikiye na ukimpata anayekuridhi nafsi yako kikweli kweli mbona utajiona malikia au mfalme japo kuwa siyo.
mapenzi hayana formular ni uvumilivu na heshima mbele na busara kichwani.

NY

Anonymous said...

si mnataka maendeleo ya technologia na kujifanya wasomi sana so hakuna noma mummy yuko kazii babayeeee yuko kazii watoto day care na babysitter mkirudi kila mmoja kisharudi kutoka kfc na burgerking biashara imeshakwisha mapenzi ya nii ya kweli ukinichengua nina wangu pembeni ananitoa baridi nipo kwa ajili ya watoto ndo maisha ya technologia na pesa mbele ya wazee wetu mnaona ya kishamba na yakizamani sasa watoto wa jingo jingo karne hii ya kizazi cha kileo cha technology vumiliyeni tu kama mwezio hakuonyeshi mapenzi ya dhati ya kweli kula kumi fungua flyer kwa wote.
maisha mpwito ngoma ya ukayeee serebuka tuu mradi unaishi hakuna wifu wala nini