Advertisements

Wednesday, November 27, 2013

KUHUSU DIAMOND PLATNAM KUHUDHURIA HARUSI YA PETER, P SQUARE HAYA NDIYO WALIYOSEMA

Mwanamuziki wa P square, Peter Okoye ameoneshwa kushangazwa na taarifa kwamba mwanamuziki wa bongo fleva Naseeb Abdul alihudhuria harusi yake hivi karibuni nchini Nigeria na kuhudhuriwa na mastaa mbali mbali akiwenmo msukumba gozi wa Totenham Hotspurs Adebayor.

Awali kupitia blogs mbali mbali kulisambaa taarifa kuwa Diamond alikua mwanamuziki pekee afrika mashariki aliyealikwa katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na tajiri nambari moja afrika, Aliko Dangote. 


Blogs hizo zilikwenda mbali kwa kumpamba diamond kwa vyeo vya ajabu ajabu ikiwemo Michael Jackson wa afrika mashariki jambo ambalo lilisababisha wengi kumponda.

 Akihojiwa na kituo cha EATV mara baada ya kuwasili jijini Dar kwa ajili ya shoo iliyopigwa viwanja vya leaders club, Okoye alishangazwa na taarifa za dimond kuhudhuria katika harusi yake. 

Okoye alikua akijibu swali aliloulizwaa na mtangazaji wa kipindi cha HotMix Adrian Hilary kuhusu diamond kuhudhuria harusi hiyo ambapo alionesha kushangazwa na jina hilo na kuhoji Diamond ni nani? 

Kushangaa huko kulimaanisha licha Diamond kujichezesha mbele ya Okoye siku ya harusi yake lakini mwanamuziki huyo hakua akijua aliyekua akimzungushia viuno vya ngololo ni nani.

3 comments:

Anonymous said...

fitini ni mbaya, mnyonge mnyongeni lakini haki yake hapewe.huyu kijana hakumiwe kwa makosa yake lakini hapewe nafasi yake pia, msimuandeme pasipo kichwa wala miguu.

Anonymous said...

Hahahaha...bongo usanii kila mtu...ndomo imekula kwake

Anonymous said...

si unaona misifa misifa ya bwana mdogo watoto wadogo always akili zao zinakuwa za kidogo kidogo lakini si wote