ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 8, 2013

KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MAXWELL MUKAMI

Maxwell Mukami wa pili toka kushoto enzi ya uhai wake

MAXWELL MUKAMI Sekunde, dakika, saa, siku, wiki, miezi, mwaka na hatimae leo Novemba 8, 2013 ni miaka kumi imetimia tangia Maxwell Mukami utangulie mbele ya haki.

Ni majonzi sana kwetu na daima utakumbukwa na ndugu zako, Baba mzazi Pascal Mukami, Mama Mzazi Mwasi Mukami, Dada yako Happyness, Kaka James Mukami na mdogo wako Octavillah Mukami

Siku zote tutazidi kukuombea baraka na pumziko jema Japo siku zote tangu ututoke tumekuwa na wakati mgumu sana,siku hii ya leo tunapoadhimisha miaka kumi ya kifo chako ni ngumu zaidi kwetu.Inaleta kumbukumbu zisizoelezeka na zisizostahimilika.

Kazi ya Mungu haina makosa.Tukijiuliza sana kwanini alikuchukua wakati bado tunakuhitaji sana tutakuwa tunakufuru.Tunajaribu kujifariji kwa kuamini kuwa alikuchukua kwa vile alikupenda zaidi yetu.Na tunajitahidi pia kujiridhisha kuwa huko ulipo unapata pumziko la amani na unaangaziwa mwanga wa milele ukistarehe kwa amani.Japo haupo nasi kimwili lakini siku zote tupo nawe kiroho.

Pumziko la Milele Akupe Ee Bwana na Mwanga wa Milele Akuangazie Ustarehe Kwa Amani,
Amen.

1 comment:

Anonymous said...

poleni sana,Mungu awape faraja mioyoni mwenu kwanu kuondokewa na mtu wa karibu kidonda kupona ni ngumu sana kwa mwanadamu,ila Mungu ndiyo muweza wa yote.