Huyu ni mchezaji wa timu ya vijana ya JKT Ruvu chini ya umri wa miaka 20, ambaye leo aliichezea timu hiyo dhidi ya Yanga katika michuano ya timu za vijana za klabu za Ligi Kuu maarufu kama Kombe la Uhai, Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam ikishinda 2-1. Hapa alikuwa anapatiwa matibabu baada ya kuumia. Je, sura hii ni ya mchezaji mwenye umri usiozidi miaka 20? Mashindano haya ni maalum kuandaa wachezaji wa baadaye wa taifa letu, ikiwa hiyo ndiyo dhamira, je tutafanikiwa? Tafakari, soka yetu inaelekea wapi kwa mtaji huu?
1 comment:
aisee mbona anaonekana ana zaidi ya miaka ishirini au ndo bongo tena kuzeeka kwa sana duuu ebwana eeh luke ahsante kila nikiingia katika blog yako naona mambo ya kunichekesha, kunielimisha kunistaajabisha na kuniliwaza ahsante mkuu mungu akubariki kwa sana
Post a Comment