ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 6, 2013

KWA WEMA WOOTE HUU NILIOMFANYIA HUYU HOUSE GIRL, HII NDIO SHUKRANI YAKE ALIYONIPA.

Ilikuwa miaka kadhaa iliyopita nilipoletewa msichana wa kazi maarufu kama house girl..ukimuangalia kwa sura alionekana mpole na mnyenyekevu.umri wake haukua mdogo sana kwani alikuwa na miaka km 20 hivi wakati huo alipofika...alipokuja alionekana wazi kuwa ametoka kwenye familia duni sana kwani hata nguo aliyoivaa ilikuwa imechoka sana.

Nilimpokea vizuri nikamfundisha kazi za nyumbani, na kumuelekeza matumizi ya vitu mbali mbali vya nyumbani kwani hakujua hata jiko la gas linawashwa vipi..Nilimfundisha mapishi mbali mbali ambayo alikuwa hajui kupika..
Alikuja akiwa na begi dogo la marlboro lililokuwa na nguo chache za kuvaa, nilimpa nguo zangu nyingi ambazo zilinibana kwani baada ya mimi kujifungua mwili wangu uliongezeka mara dufu...nikamfundisha usafi wa kuoga asubuhi na jioni ili awe smart na aweze kukaa na watoto akiwa msafi.

alikuwa msikivu na hakuwa mjeuri, niliishi naye kama ndugu yangu na hakika ungenikuta nae tunavyopiga stori usingedhani kama ni house girl kuna watu walijua yule ni ndugu yangu kwa jinsi tulivyokuwa tunapatana....nikiwaambia ni house girl hawaamini..

Tuliishi kwa vizuri na hatukuwahi kugombana hata siku moja kwani kwa kiasi kikubwa alitimiza majukumu yake niliyompangia.

Baada ya muda nikaona nimsaidie zaidi kwani pamoja na kuwa ni house girl wangu lakini pia alikuwa yatima kwani wazazi wake wote walishafariki dunia..Na pia mtoto wangu wa mwisho kwa wakati huo alianza shule kwa hivyo angepata fursa ya kujiendeleza kwani hakukuwa na mtoto mdogo aliyebaki nyumbani..

Nikamtafutia shule ya Qualify Test ili asome masomo ya sekondari ambayo nilimgharamikia kila kitu..akaanza kusoma hiyo shule kwa makubaliano kwamba atafanya kazi zake zote asubuhi na mchana aende shule..

Nilipokuwa nasafiri na watoto wakati wa likizo au kwenda mapumziko mikoa mbali mbali au nje ya nchi naye pia nilimchukua tukawa pamoja naye..(kumbuka kuwa hapo nyumbani kwangu nilikuwa naishi na watu wengine ambao ni ndugu zangu lkn niliwaacha wao nikawa namchukua yeye)
Kila nilipokuwa nasafiri kikazi nilikuwa nawaletea watoto wangu zawadi na yeye pia namletea..

Wakati wa sikukuu nilikuwa nawanunulia watoto wangu nguo mpya na yeye pia namnunulia..na ili kumfanya ainjoi sikukuu yake zaidi nilikuwa nampa pesa ambayo simkati kwenye mshahara wake..

Kila Jumapili alikuwa free kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni, nilimruhusu aende popote lakini ikifika saa 12 awe kesharudi..
Kila mwisho wa mwaka nilimpatia nauli na zawadi za kuwapelekea ndugu zake na wadogo zake na alienda likizo
Nilimkatia bima ya afya na yeye akawa anatibiwa Aga Khan hospital kama watoto wangu.

Nilimnunulia simu ya mkononi na kila simu yake ilipoharibika nilimnunulia nyingine
Kabla sijanunua machine ya kufulia aliniambia yeye hawezi kufua nguo na mikono kwani mikono yake inaharibika na kupata fangas nikamtafuta mtu wa kufua nguo ambaye nilikuwa namlipa..

Kila alipofanya kazi ya ziada kwa mfano kuhudumia wageni au siku za sikukuu ambapo kazi ni nyingi nilikuwa namlipa pesa muda huo huo baada ya kumaliza hizo kazi, na mshahara wake mwisho wa mwezi uko pale pale..

Siku moja moja za wiki endi nilikuwa namsuka kwani kwa bahati nzuri mie najua kusuka mitindo mingi tu...
siku kama sijamsuka basi nampa hela ya saluni/msusi
siku nikienda naye sokoni/supermaket basi hanunui chochote kwa pesa yake, akitaka kitu namnunulia
kila mwaka unapoisha na mwaka mpya kuingia nilikuwa namuongeza mshahara ili naye ajisikie mwenye thamani.

Kwa muda niliokaa naye aliweza kusave na kununua plot baada ya mimi kumshawishi afanye hivyo ili iweze kumsaidia baadae, japo mimi nilimuongezea pesa kidogo iliyopelea.
Nilimuahidi kumsomesha hadi chuo kama yeye angependa na kujitahidi katika masomo ili naye awe na maisha yake baadae..

kichwani mwangu nilipanga kumfundisha gari kwani nilishamchukulia km ndugu yangu...hili nilikuwa sijamwambia, nilitaka amalize kwanza elimu ya sekondari.

NOTE
kwa nature ya kazi yangu huwa nasafiri mara kwa mara lkn nikiwa nyumbani lkn huwa sina tabia ya kujibweteka na kumuachia house girl afanye kila kitu...

Kila siku jioni napika chakula cha usiku baada ya kurudi kazini, nikichelewa namwambia apike cha watoto na watu wengine, changu na cha baba napika mwenyewe nikifika...mara nyingi mimi na mr tunakula ugali wao wanapenda wali, n.k
nafanya usafi wa chumba changu choote hadi washroom mara 3 au 4 kwa wiki nafua nguo zangu na za mume wng zote siku ya jumamosi.

siku ya jumamosi na jumapili naingia jikoni kuanzia asb hadi jioni, except kama nimeenda kazn au nimepata dharura..siku za wk end asb huwa natengeneza mchemsho kwa ajili ya familia....na pia napika mwenyewe chakula cha mchana na usiku..(binafsi huwa sipendi kupikiwa hasa nikiwa nyumbani kwani nahisi km chakula kina kasoro nyingi km atapika m2 mwingine,) kwa ivo huwa naingia jikoni mwenyewe.

ALICHONIFANYIA SASA
Baada ya miaka kadhaa nikahisi kama anabdilika na kuwa jeuri lkn sikujali saana, nilijua tu labda yuko days hivi ambayo wkt mwingine yanasababisha mood kuchange..
Nilikuwa na mpaka leo huwa simruhusu house girl kuingia chumbani kwang kwani usafi na kila kitu huwa nafanya mwenyewe hata kama nina mimba ya kujifungua leo..

Sasa kuna kipindi niliposafiri nilikuta kitanda changu kimetandikwa vizuri mpk nikawa na was was, sababu mume wangu huwa hatandiki wala habadilishi shuka mpaka nirudi safari...Siku moja nilimuuliza mume wng nani kamtandikia kitanda? kwani najua kbs hata km ni yeye katandika hawezi kunyoosha shuka vizuri, mara nyingi mume wng yupo rafu, akaniambia amemuomba house girl amsaidie kutandika, nikamuuliza tangu lini house girl anaingia chumbani kwng? akasema samahani mke wng sitarudia tena...nikanyamaza moyoni nikaanza kuwa na shaka lkn sikufatilia saana... huyo house girl siku zooooote hakuwahi kuingia chumbani na mimi sijawahi mruhusu, iweje kipindi hicho tena nikiwa nimesafiri aingie? hapo alikuwa kashakaa muda wa kutosha na keshakuwa mzoefu ila sio chumbani kwangu...ila nikapotezea kwani baada ya hapo ikawa hata nikisafiri nakuta vile vile chumba kipo rafu rafu, hakujatandikwa kama zamani, nikajua ni kweli ilikuwa msaada tu kwa mr na nikafutilia mbali wasi wasi wangu...

Miezi miwili baadae huyo house girl akaniaga ghafla akisema bibi yake ni mgonjwa anaumwa, kwa sababu nilikuwa na namba za simu za ndugu zake nikawauliza wakasema kweli bibi yake anaumwa, nikamruhusu aende kumsalimia..akaondoka, lkn kilichonishangaza ni pale alipokusanya mabegi ya nguo zake zote, viatu vyake vyote n.k nikamuuliza mbona umekusanya kila kitu hutegemei kurudi? akasema anaenda kuwagawia ndugu zake yeye ataanza upya akirudi..na vile alikuwa bado anasoma sikumtilia shaka nikajua atarudi tu...

alipofika kwao tu akanitumia ujumbe mfupi wa simu akisema yeye hatarudi tena na ameamua kusomea huko huko kwao.....aaaaaaaaaahhhhhhhhhhh nilikuwa so much dissapointed sababu wakati huo mi nilikuwa mjamzito tena nakaribia kujifungua...kuna ndugu yng alinionea huruma akaniletea msichana wake anisaidie...

Baada ya muda nikasikia yule house girl wangu aliyeondoka ni mjamzito, sikufatilia ila nikajua ndio sababu iliyomfanya aondoke nyumbani kwangu..

Baadae akajifungua nikaambiwa, nami nikampigia simu kumpongeza, na pia nikamnunulia zawadi za mtt nikampa mtu ampelekee...lakini pia mara kwa mara nilikuwa nampigia cm na kumsalimia yy na mwanae..
MIAKA KADHAA BAADAE ndio nikaja kujua kuwa huyo mtt wa house girl wangu ni wa mume wangu...
Nilipomuuliza mume wangu alikubali na kuniomba msamaha saaaana, akasema huyo house girl kila nilipokuwa nasafiri alikuwa akivaa kanga moja na kujilengesha sana mpk akaingia kwny mtego.

SIWEZI SEMA, MAUMIVU niliyopata hayaelezeki.....
NI MIAKA KADHAA imepita toka tukio hili kutokea, lkn mpaka sasa bado nasikia maumivu yake moyoni....in fact ht jana uck nilikosa usingizi baada ya kukumbuka tukio hili, nikajikuta machozi yananitoka bila kuyazuia...

kwa wema wooooote niliomfanyia huyu house girl kweli hii ndio shukurani yake?,yaaani sina hamu..na mpk leo hii sina hamu...nilibaki nimeshikwa na butwaa..
japo hiyo haijanifanya niwachukie mahouse girl wengine lakini sina hamu nao kabisa hawa watu.

10 comments:

Anonymous said...

mtu wa kumlaumu ni mumeo pia, kwani it takes two to tango.

Anonymous said...

Hasira zako unaelekeza kwa mtu asiye sahihi. Naamini wewe hukuwa na mkataba wowote na house girl wako kuhusu kutohusiana kimapenzi na mumeo. Ila naamini pia wewe na mumeo mna mkataba labda wa kimaandishi kuwa anapaswa kuwa na wewe tu na si mwingine. Kwa hiyo basi tatizo lako sio HOUSE GIRL bali ni kwa MUMEO. Hatuwezi kuweka mikataba na WATU fulani na KUTEGEMEA mikataba hiyo itaheshimiwa na watu wengine ambao hatuna mikataba nao bali tunategemea watekeleze majukumu yaliyo ndani ya makubaliano yasio wahusu.

Anonymous said...

You deserve it. It just shows how naive you are by blaming the wrong person, Aliyekukosea mmeo. Kwani kuona kanga ndio suruali hudondoka? Wanaume wangapi tunao mahaus girl na ujinga huo hatufanyi. I fee sorry for the poor girl, some how for you as well but the real culprit here is your husband. Throw him away.

Anonymous said...

Blame your husband, housegirl was only following orders.

Anonymous said...

Pole sana Dada kwa yote. Ila Mimi sioni ubaya WA house girl na hujui ni katika mazingira gani yaliyompata pengine kalazimishwa. Mimi naona WA kumlaumu zaidi ni mume wako kwa kitendo alichokifanya kwa binti WA watu tena yatima. Wewe ubarikiwe kwa kumsaidia huyo binti. Ila cha msingi samehe na uanze upya

Anonymous said...

sawa house girl anamakosa lakini Mumeo nae anamakosa sana sana kwa sababu angekuambia kua kila ukiondoka huyu msichana ananitia majaribuni. Pia ulipolalamika kua kitanda kimetandikwa wakaona basi wachezee hapo bila kutandika tena. Wanaume nao ni mbwa kabisa. kama unavyodharau wasichana wa kazi ujue pia na Mumeo hakua na haki, inamaana kila akiona mwanamke nusu uchi lazima amuingie? kakukosea heshima huyo bwana nayeye usimuachilie kiurahisi inabidi ajifunze!!!!1.

Anonymous said...

Pole sana kwa hayo yaliyokukuta. Ahsante pia kwa kutupa somo hili, tumejifunza mengi kwa story hii, ningependa tuwasiliane kama utaweza ili unipe ushauri sbb nahisi umejifunza mengi. email yangu ni mwehuu13@gmail.com

Anonymous said...

Sitaki kujua umri wako ila nahisi wewe ni mdogo wangu ki umri usia kwako na kwa wengine wote kutokana na uzoefu nilionao mume ambaye ametembea na house girl mmoja hatoishia kwa huyo tu ina maana kila house girl atatembea naye bila ya wewe kujua na baadae atatembea na ndugu zako pia mchunge hata kwa wanao samahani sana kusema hivyo imeniuma saana kama ni mimi niliyefanyiwa, halafu visingizio ni hivyo hivyo wote huwa wanadai at hgirl kamtaka mara kanga ilimwanguka mbele yake mara shanga zilionekana, usimlaumu mteme uishi kwa amani ila angalia kuhusu watoto usije ukawaathiri kisaikolojia vinginevyo kila mmoja na chumba chake mlee watoto chunguza katembea hata na majirani au watoto wa jirani najua hutoamini ila kuna ukweli ndani yake, pole sana mdogo wangu lawama zooooooote mpe mumeo

Anonymous said...

Dada pole kwa yaliyokukuta,unaonekena ni Mstaarabu sana pole tena usijilaumu kwa wema wako hivi ndivyo tunavyotakiwa tuwe binadamu.Mimi nafikiri mkosa ni mume ila mama jaribu kusamehe muanze kurasa mpya haina maana mumeo ndiyo kawaida yake msamehe mlee watoto wenu na msamehe huyu mfanyakazi maana uelewi mumeo alimwambia nini ni ngumu lakini is possible pole sana mama

Anonymous said...

POLE KWA YALIYOKUKUTA DADA. STORY YAKO INAMAFUNDISHO, LAKINI WA KULAUMIWA NI MUMEO HE SHOULD HAVE KNOWN BETTER! THAT SAID: HE HAS TO SUPPORT THAT BABY REGARDLESS! MWENYEZI MUNGU AKUPE NGUVU KWA KUMSAIDIA HUYO HOUSE GIRL APATE ELIMU NA MENGINEYO KWANI SIYO WATU WOTE WANA MOYO KAMA HUYO...NA ILBIDI AKUHESHIMU FOR THAT!