Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Diwani Athumani (wa kwanza kushoto) akiangalia mwili wa marehemu Kassim Siadi katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya. Pipi 65 za dawa zinazodaiwa kuwa za kulevya zimekutwa tumboni mwa marehemu wakati pipi moja kati ya hizo ikiwa imepasuka.
Passport ya marehemu Kassim Saidi.
Nguo pamoja na baadhi ya vitu alivyokuwanavyo marehemu Saidi.
ACP Diwani Athumani akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
Maofisa wa Polisi wakikagua pipi zilizokutwa tumboni mwa marehemu.
(PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG)
- MNAMO TAREHE 07.11.2013 MAJIRA YA SAA 11: 00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. KASSIM SAIDI MBOYA, MIAKA 36, MKAZI WA DSM ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. MAREHEMU ALIFAHAMIKA JINA KWA MUJIBU WA HATI YAKE YA KUSAFIRIA NAMBA – AB 051010 KUTOKA DSM KUELEKEALILONGWE NCHINI MALAWI.
-MAREHEMU ALIKUWA ANASAFIRI AKIWA KATIKA BASI LA TAQWA LENYE NAMBA ZA USAJIRIT.319 BLZ AINA YA NISSAN KWA MUJIBU WA TIKETI YAKE ILIYOKUWA NA JINA LA KASSIM MUECK MICHAEL, AKIWA NA BEGI DOGO LENYE SURUALI MOJA AINA YA JEANS,T-SHIRT MOJA NYEUSI,RABA JOZI MOJA RANGI NYEKUNDU,MKATE MMOJA ,MKOBA MDOGO WA KIUNONI,VACCINATION CARD MBILI ZA KINGA YA UGONJWA WA MANJANO, RANDI MBILI SARAFU ZA AFRIKA KUSINI NA MIFUKO SITA YA RAMBO RANGI NYEUSI.
-AWALI BASI HILO BAADA YA KUFIKA MPAKANI KASUMULU NA ABIRIA KUSHUKA KUTOKA KWENYE GARI HILO NA KUANZA KUFANYA TARATIBU ZA KUVUKA MPAKA KUINGIA NCHINI MALAWI, MAREHEMU ALIBAKI NDANI YA GARI HUKU HALI YAKE YA KIAFYA IKIZIDI KUDHOOFIKA.
-WAHUSIKA WA GARI WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI AMBAPO MAREHEMU ALICHUKULIWA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA KWA MATIBABU. HATA HIVYO KABLA HAJAPATA MATIBABU ALIFARIKI DUNIA.
-KUFUATIA DALILI ALIZOKUWA NAZO KABLA YA KUFARIKI ILIBIDI MWILI WA MAREHEMU USAFIRISHWE HADI HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA KUFANYIWA UPASUAJI AMBAPO ZILIPATIKANA PIPI 65 ZA DAWA ZIDHANIWAZO KUWA ZA KULEVYA ZIKIWA TUMBONI KWA MAREHEMU NA MOJA KATI YA PIPI HIZO IKIWA IMEPASUKA.
-TARATIBU ZINAFANYWA ILI DAWA HIZO ZIPELEKWE OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI KWA UCHUNGUZI WA KITAALAM IKIWA NI PAMOJA NA KUJUA AINA YA DAWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO.
-KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA KWANI SIO TU NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI BALI PIA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA RAI KWA WAKAZI WA MBEYA NA TANZANIA KWA JUMLA KUFIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA AJILI YA UTAMBUZI WA MWILI WA MAREHEMU.
IMETOLEWA NA:
[DIWANI ATHUMANI- ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
5 comments:
inalilah wainailah ilah raj un...marehemu mmesema vitu alivyokuwa navyo mbona hamkutaja pesa inamaana hakua na hata centi mfukoni
wamesema ebu some na wewe ..alikuwa ana hela za afrika kusini
kweli kabisa wasema hizo pesa zipo wapi na cha pili ni kwamba mbona hawatajwi wanauwatuma hawa vijana wako wakuu wanawatuma hawa kama punda wao wamekaa na watoto wao wakifaidi matunda ya hawa walala hoi na wala hawakamatwi tujiulize inakaaja hii kitu kila leo ukisoma story hizi unaonyeshwa walala hoi kukamatwa au kufa wakuu wamepoa majumbani na maofisini mwao na wala hawaguswi how come
Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peopni.
Hivi kuna haja ya kupiga picha pasort yake na kuibandika kwenye mitandao?
Wanaowatuma watatajwa vipi nanwao ndio washika mpini? Wao ndio wenye serekali, wanaiba serekalini na huku wanafanya biashara haramu. Hawatosheki na hawatotosheka mpaka wataingia makaburini mwao.
Post a Comment