Sunday, November 24, 2013

MH MBUNGE WA BUMBULI AFUNGUKA NA KUSEMA KUMSHAURI ZITTO HAYA

Mbunge wa Bumbuli -CCM na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh Januari Makamba 
*Chini ni Tweet ya Mheshimiwa January Makamba Muda Mfupi baada ya Kamati Kuu ya Chadema Kumvua Nyadhifa Zitto Kabwe
Yakiwa masaa kadha yamepita Toka Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kumvua Nyazifa zake zote Mbunge wa Kigoma Kaskazini na kumpasiku kumi na nne ajieleze Sababu zitakazomfanya asifutwe kabsa Wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo baada ya kukiuka Utaratibu wa Chama.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh Januari Makamba amefunguka na kumkaribisha Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kambwe kujiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi (CCM),January Makamba amefunguka katika Mtandao wake wa kijamii na kusema kuwa kama Viongozi wa Chadema Hawatambui na kuona dhamani ya Kiongozi hiyo hivyo akaribie CCM.
“Kama wenzako hawathamini kazi kubwa uliyofanya kukijenga Chama chenu na kazi unayofanya Bungeni, karibu CCM tuijenge nchi.”

2 comments:

Anonymous said...

January, wewe ni muhuni hujui usemali kwani CCM wamewafukua wangapi na hapa juzi kuna watatu NAPE amedai wavuliwe uongozi!! Acha hizo wewe. hutufai.

Anonymous said...

Kwani CCM inajenga nchi?