
MWANAMUZIKI MATONYA
Mwanamuziki nyota wa muziki wa kizazi kipya usiku wa kuamkia Jumatatu alionja joto ya kiwe baada ya kutekwa na kusurubiwa kisha kunyang'anywa kila kitu pamoja na gari yake.XDEEJAYZ inakupa mchongo mzima.
Mwanamuziki huyo akiwa kwenye viunga vya Club ya usiku ya Kibo iliyopo Tegeta Jijini Dar pamoja masisita du wakila bata ghafra kundi la watu watano lilimvamia na kumkamta msobe msobe hadi nje ya ukumbi pamoja na kumrukisha kichurachura huku wakina dada waliokuwa wamendamana nao wakilia kwa uchungu kwa kumuonea huruma.
Habari zaidi toka kwa chanzo chetu cha Xdeejayz kilichoshuhudia timbwiri hilo kilisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni kudaiwa kwa Matonya na mtoto wa mjini aliyefahamika kwa jina la Evance" Huyu Evance ni mtoto wa mjini na huwa anawakopesha pesa wanamuziki mbalimbali pamoja na wasanii wa bongo movie hivyo miezi ya hivi karibuni alimkopesha shilingi laki nne msanii huyo kwa madai kuwa hakuwa na pesa ya kula bata wikiendi ambapo baada ya kumkopesha msanii alianza kuzungusha kurudisha hali iliyomfanya Evance kuchukua hatua za kumfanyia unyambilisi huo" Kilisema chanzo chetu
Hata hivyo baada ya kumkamata msanii huyo Evance alimpelekwa Oysterbay ambapo aliiacha gari na simu kwa makubaliano atakapoleta pesa hiyo atapewa gari yake.
Bongo Clan
2 comments:
hawa mastaa wa bongo sasa watajifunza,wanataka kujifananisha na mastaa wa mtoni kazi kutangaza mali zao kwenye mitandao mm napata pesa hizi na magari manne ukimuuliza anakaa wapi uswahilini na nyumba yenyewe mlizi mmasai hamna camera wala nn?,pata pesa zako nyamaza sio unataka kuweka maisha yako hatarini,mdau USA
umesema kweli mdau wa usa nakuunga mikono na miguu yangu yote nakupa kumi mwanangu wanapenda sana sifa sifa za kijinga jinga halafu wengi wao ukiwaona hivi na misifa misifa hawajawahi kushika pesa maishani mwao so wanapata kiwewe hawaamini na kuwaona wenginewe wajinga kujiona wao ndo wamepata
lakini tusiwalaumu sana ndo hulka ya maskini akipata matako hulia mbwataaa human psychology hiyo ya kimaskini ukipata unajitapa na kujitangaza kama kashata ya mataaa
ya upanga osterbay mbezi.
mdau NY BABY
Post a Comment