Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabia Nchi wa COP19/CMP9 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Poland, mjini Warsaw. Rais Kikwete alikuwa anazungumza kwa niaba ya viongozi wa Umoja wa Afrika (AU) katika nafasi yake akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi (CAHOSCC).
Rais Kikwete amekuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo tokea Januari, mwaka huu, 2013, wakati alipochaguliwa na viongozi wenzake kushika nafasi hiyo kufuatia kifo cha aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mheshimiwa Meles Zenawi, Septemba, mwaka jana.
Picha na Ikulu
THE UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
ataja hatua saba kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amependekeza hatua saba za msingi za
kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kupunguza uzalishaji wa gesijoto na
kuongeza fedha za kukabiliana na hali hiyo duniani.
Aidha, Rais
Kikwete amesema kuwa ni siri ya wazi kuwa Afrika inateseka zaidi kwa kukabiliwa
na changamoto nyingi na za kila aina kutokana na mabadiliko ya tabia nchi
pamoja na ukweli kuwa inachangia kidogo sana katika kuzalisha gesijoto na kuharibu
mazingira.
Akizungumza
kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabia Nchi wa
COP19/CMP9 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Poland, mjini Warsaw,
jioni ya leo, Jumanne, Novemba 19, 2013, Rais Kikwete amewaambia mamia ya
washiriki wa Mkutano huo kuwa dunia inahitaji kuchukua hatua saba za msingi
kukabiliana na hali hiyo.
Hatua hizo ni zifuatazo:
(a)
Kukubaliana
kuhusu njia za msingi za kitaasisi za jinsi ya kuzifidia nchi kutokana na
upotevu unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi.
(b)
Kukubaliana
kuhusu ni taasisi ipi itasimamia shughuli zinazohusiana na misitu. Taasisi
itakayohakikisha na kusimamia namna ipi nchi masikini zinavyoweza kufidiwa
kifedha kutokana na upunguzaji wa gesijoto.
(c)
Kukubaliana
kuhusu misingi, masharti na maelekezo ambayo yatasimamia hatua za kupunguza
gesijoto katika nchi zilizoendelea.
(d)
Hatua
na njia ambazo zitaongoza nchi zilizoendelea kupunguza gesijoto zinatakiwa
kukubaliwa na kuelezwa waziwazi.
(e)
Kuna
umuhimu wa haraka wa kuupatia Mfuko wa Mazingira wa Kijani fedha za kuanzisha
na kuimarisha Mfuko huo. Kwa sasa ni Mfuko mtupu. Lazima tuhakikishe kuwa
unajazwa ipasavyo. Aidha, lazima tukubaliane namna gani kiasi cha dola za
Marekani Bilioni 100 zilizokubaliwa kuchangwa kila mwaka zitakavyopatikana na
kugawanywa.
(f)
Kituo
cha Teknolojia ya Mazingira na Mtandao kitafute jinsi ya kuondoa vikwazo katika
masuala yanayohusiana na uhamishaji wa teknolojia kutoka nchi tajiri kwenda
nchi zinazoendelea na kumaliza changamoto zinahusiana na Haki Miliki.
(g)
Kwenye
COP hii tunahitaji kukubaliana kuhusu baadhi ya mambo yanayohusiana na
upunguzaji wa gesijoto.
Rais Kikwete
alikuwa anazungumza kwa niaba ya viongozi wa Umoja wa Afrika (AU) katika nafasi yake akiwa Mwenyekiti
wa Kamati ya Viongozi wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi (CAHOSCC).
Rais Kikwete
amekuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo tokea Januari, mwaka huu, 2013, wakati
alipochaguliwa na viongozi wenzake kushika nafasi hiyo kufuatia kifo cha
aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mheshimiwa Meles
Zenawi, Septemba, mwaka jana.
Viongozi
wengine ambao wamezungumza katika Mkutano huo wa ufunguzi ambao Mwenyekiti wake
alikuwa ni Rais wa COP 19 Mheshimiwa Marcin Korolec, Waziri wa Mazingira wa
Poland ni Waziri Mkuu wa Poland, Mheshimiwa Donard Tusk na Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki Moon.
Wengine ni
Rais wa Mkutano wa 68 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Balozi John
Williams Ashe ambaye ni Balozi wa Antigua na Barbuda katika Umoja wa Mataifa na
Katibu Mtendaji wa Mkataba wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi wa Umoja
wa Mataifa (UNFCC), Mheshimiwa
Christiana Figueres.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
19 Novemba, 2013
No comments:
Post a Comment