ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, November 10, 2013

SHUKRANI KWA UPENDO NA UMOJA MLIOONYESHA KATIKA MSIBA WA MARTHA SHANI

 SHUKRANI
Na Alex Kassuwi
DMK, Alex Kassuwi na Davis Mosha wakisubiri mwili wa Martha Airport October 30, 2013

Ndugu zangu hadi hivi sasa siamini yaliyotokea, bado haijaingia akilini kama mke wangu mpenzi
Martha Shani hatunaye tena! Siamini kama Martha amefariki! Naona yupo. Ndugu zangu kwa sasa nipo katika kipindi kigumu sana, nikiwa mwenyewe nikiangalia watoto machozi yanitoka. Maneno ya kinywa changu hayawezi kuelezea kuugua kwa nafsi na roho yangu. Ndugu zangu, |Mama zangu, kaka zangu, dada zangu, mashemeji zangu, wakwe zangu, marafiki na jamaa zangu  pamoja na yote haya sina budi kutoa shukrani zangu kwa yote mliyonitendea kuanzia maombi hospitali, kuwa nasi kipindi chote cha msiba mpaka kuusafirisha na kuuhifadhi mwili wa mpenzi wangu nyumbani Tanzania ambapo tulizika Alhamis Oktoba 31,2013 huko Puma Singida.


shukrani ZA PEKEE kwa ubalozi wa tanzania nchini marekani
Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani.


Natoa shukrani za pekee kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa kuwezesha makaratasi ya kuusafirisha mwili wa mpenzi mke wangu.
Shukrani kwa wafanyakazi wote wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa kutununulia tiketi tatu za ndege, mimi na watoto wangu wawili.
Shukrani za pekee kwa Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Familia yake, kwa kuwa nasi kuanzia siku ya msiba hadi mwisho, na kuwahamasisha watanzania wote bila kujali dini,itikadi za kisiasa wala ukabila.



shukrani kwA VYOMBO VYA HABARI
Navishukuru sana vyombo vyote vya habari vilivyoshiriki kuhabarisha juu ya msiba huu. Vyombo ni vingi sana siwezi taja majina ya vyombo  vyote nafasi haitoshi, nawashukuru sana wanahabari wote. Bali sina budi kutoa shukrani za pekee kwa Swahilitv blog, DJ Luke wa Vijimambo blog, Mubelwa Bandio wa Changamoto yetu blog, Abou Shatry wa Swahilivilla blog, Sundayshomari blog, Lucy Patrick blog, DMk411 blog na Issamichuzi blog kwa kuweza kuwahabarisha watanzania wote.

SHUKRANI KWA WACHUNGAJI
Mch. Peter Igogo – Cathedral of Praise Church, Bowie, MD
Mch. Ferdinand Shideko – The Way of the Cross Gospel -|College Park, MD
Mch. Mathayo Malekela  Asssemblies of God –Georgia Ave, Silverspring, MD
Bishop Melchizedeck Maturlo  Bethel Kingdom Church- Hyattsville, MD
Mch. Solomon Ng’imba kutoka Double Oak Community Birmigham Alabama
Mch. Nicodemus Hanje Kutoka Birmigham Alabama
Mchungaji Jerry Price  International Community Church

shukrani ZA PEKEE kwa kamati ya mazishi marekaniNatoa shukrani za pekee kwa kamati nzima ya Mazishi Marekani ikiongozwa na Mwenyekiti Bw. Augustino Malinda.

SHUKRANI ZA PEKEE WATU BINAFSI MAREKANI
Natoa shukrani za pekee kwa Bw. Neto na Mkewe Bi. Kate kwa kuwa nami nyumbani walifika mara moja alipoanguka mke wangu, tumekaa wote hospitali masaa nane pamoja hadi mwisho, wengine waliofika hospitali ni 
Bw.  MK (Dickson Mkama), Mrs. Mohamed, Bora, Bw. Julius Manase na Mkewe, Mchungaji Mathayo Malekela, Mchungaji Peter Igogo, Mch. Jerry Price, , Augustino Malinda, Jack, Mariamu na Mvuniwa, Dada Faith Isingo,  Pamela Gea, Kwizera, Sekela, Jack Odong na wengine wengi siwakumbuki majina.
Shukrani pekee kwa Cedra Eaton na Mumewe Bw. Honesty Mulamula

SHUKRANI KWA WANAMAOMBI

Ndani na nje ya Marekani: 
Dada Nancy Mosha, Alex Dago Motion, Ruth Shani, Neto Mwimbwa, Kate, Mrs. Mohamed, Bora, Julius Manase na Mkewe, Mchungaji Mathayo Malekela, Mchungaji Peter Igogo, Mch. Jerry Price, Augustino Malinda, Mary Mgawe,Jack, Mariamu na Mvuniwa, Dada Faith Isingo, Kwizera, Sekela, Jack Odong, Theresia Kassuwi, Martha kilimba, Neema Shani, Joseph Shani, Noel Shani na Wana maombi wote.

shukrani ZA PEKEE kwa kamati ya mazishi TANZANIA
Natoa shukrani zangu za dhati kwa kamati ya Mazishi ya Tanzania ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati  Bw. Hamis Mpinda.


SHUKRANI ZA PEKEE WATU BINAFSI TANZANIA
Alex Kassuwi, Davis Mosha, Muddy na Masanja Mkandamizaji

Natoa shukrani maalum kwa Davis Mosha na Mkewe (Dada Nancy) kuwa nasi bega kwa bega kuchangia kwa kiasi kikubwa kuusafirisha mwili wa mpenzi mke wangu toka Marekani hadi nyumbani Tanzania, Muhimu zaidi familia ya Davis Mosha wamekuwa faraja kubwa sana kwangu na kwa watoto wangu kwa msaada, upendo walionao na malezi kwa watoto wangu. Asante sana Davis Mosha na Dada Nancy.

SHUKRANI ZA PEKEE KWA WAFANYAKAZI WA UBALOZI WA MAREKANI TANZANIA, USAID NA CDC
Dada Olivia, Alex na Dada Georgia
Dada Olivia, Alex na Dada Georgia. Walipokuja nipa pole na kuwakilisha rambirambi za wafanyakazi wa Ubalozi wa Marekani Tanzania .
Wafanyakazi wa Ubalozi wa Marekani walikuja msibani. Kutoka kushoto; Bw. Tairo,Mushi, na MarkD

NATOA SHUKRANI MAALUM KWA
Bw. Hamis Mpinda na marafiki zake Bw. Dan Fundisha Ezekiel 
Bw. John Langas
Bw. Vincent Mughwai
Wafanyakazi wa Ubalozi wa Marekani Tanzania
Wafanyakazi wa NHC Makao Makuu
Bwana na Bi. Ridhiwani Kikwete kwa msaada wao na upendo kwa watoto
Diwani wa CCM kata ya Pangani Kibaha Bi. Mwanaidi Maliki Kiongoli
Diwani wa CCM Puma Mhe. Ramadhani Kulungu
Diwani Ikungi CCM viti Maalum Mama Asha Mnjori
Kanisa la Pentekoste Puma
Mchungaji Peter Ihema wa kanisa la Kanisa la Pentekoste Puma,

shukrani ZA PEKEE kwa taasisi TANZANIA
1. nssf
Nawashukuru sana shirika la NSSF kwa kuweza kuchangia kusafirisha mwili wa mpenzi mke wangu Martha Shani.
Bi. Eunice Chiume na
Bw. Crescentius Magori


2. IDEA ( Ikungu  Development Association)
Nawashukuru sana wanachama wa IDEA kwa upendo na msaada wao.

3. SHAMBOGO FOUNDATION
Shukrani za pekee kwa shambogo Foundation kwa kushiriki kikamilifu katika msiba wa mpenzi mke wangu.


mWISHO NATOA SHUKRANI KWA WATANZANIA WOTE WA NJE NA NDANI YA NCHI KWA MOYO WA UPENDO NA USHIRIKIANO

3 comments:

Anonymous said...

Pole sana wafiwa, mungu aendelee kukupa nguvu pamoja na familia yako, kazi ya mungu haina makosa, pole sana kaka Alex

Anonymous said...

Jamani mie naangalia tu huyu mtoto natoka machozi. sijui hata anafikiria nini hapo. hamuoni mama labda anasema maam kaenda kazini nitamuona soon ila wapi too sad jamani. Poleni sana wafiwa. walio karibu muwe mnasaidia huyu baba watoto ili aweze kwenda kazini.

Anonymous said...

kweli imenisikitisha sana hapo anavyosema siamini kama ni kweli mke wangu sipo nae na nikiangalia watoto machozi yananitoka....Alex kweli kidonda chakufiwa na mtu wakaribu kupoa au kupata jibu ni kweli imetokea ni ngumu sana cha zaidi uishi kwakumtegemea tu Mungu ndio muweza wa kukupa faraja bila yeye hutaweza kitu,pole sana sana.