
Mbunge wa viti maalum kutoka mkoa wa Mara, Ester Amos Bulaya amesema ataendeleza vita dhidi ya mtandao wa wafanyabiashara wa madawa ya kulevya nchini licha ya kupokea vitisho kuwa anaweza kuuawa.
Mbunge huyo alitoa hoja bungeni kuitaka serikali kufanya mabadiliko ya sheria ya dawa za kulevya na kuanzisha mahakama maalum ya kushughulikia wahalifu wa dawa za kulevya.
“Nimepata maoni mbalimbali ya kwenye mitandao,simu nimetumiwa meseji za kufurahisha na kunitia moyo. Lakini kuna baadhi ya wachache ambao wanakuwa na hofu kuniambia ‘watakuua, watakutaka kucha’ something like that. Lakini nilicho waambia hatuwezi kuacha kusema vitu vya msingi ambavyo vinagusa taifa letu,vinachafua taifa letu katika anga za kimataifa.Lakini hatuwezi kuacha kuzungumzia mtandao wa madawa ya kulevya eti kwasababu wanaoneka ni untouchable ni watu wenye fedha,” alisema
No comments:
Post a Comment