Wafanya biashara wa Mkoa wa Morogoro wakiwa wamekusanyika wakijadili jambo.
Wafanyabiashara wa Mkoa wa Morogoro wamegoma kufungua maduka leo wakitaka kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa Lengo la kushinikiza kukataa mashine za kieletroniki za mamlaka ya mapato tanzania.Wafanya biashara hao wamegoma kufungua maduka tangu asubuhi wakishinikiza kuonana na mkuu wa mkoa jambo ambalo Mkuu wa mkoa amekubali na kuwaomba wateuliwe wawakilishi 8 kwa ajili ya kwenda kuonana nao.Baada ya wawakilishi kuteuliwa bado wafanyabiashara hao walishinikiza kuandamana mpaka nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa ndipo Jeshi la Polisi walipoingila kati .
Jeshi la Polisi wakiwa katika barabara inayoelekea Kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Kulinda Amani na kuzuia maandamano yaliofanywa na wafanyabiashara hao muda huu.

maduka yakiwa yamefungwa katikati ya Mji wa Morogoro
Wafanyabishara hao wakiandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kushinikiza kuondolewa kwa mashine za Kieletroniki kwa madai kwamba ni kikwazo kikubwa katika biashara zao .
Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia hapa picha kwa hisani ya Morogoro Yetu Blog.



4 comments:
Jamani waTanzania na wanaMorogoro, wafanyibiashara, je fanymnataka kuendelea kutokulipa kodi hadi lini?? tuache kutoelewa tecknolojia inakoelekea! Hizi mashine mnaziogopa kwa sababu gani? kwanza muelewe zinawasaidia kudhibiti biashara yenu kwa ufanisi zaidi. Elimu ya biashara hamna ndio tatizo hilo. Tukubali mabadiliko.
Sasa we ndio juha kweli hakuna anaekataa kulipa kodi kama hujui uliza tra kama wanataka wawapatie hizo mashine bure hslafu uone watu aatakataa mashine ikunufaishe wewe tununue sisi hiinimetoka wapi
mabadiliko pia wakuu nao wakubali siyo kuchukua pesa zetu na kula na familia zao mabadiliko yawe kwa pande zote mbili msituyayushe bwana tumeshaamka msituone wajinga hatutaki technologia hii ila tumeshaona mbali haina faida na sisi ila kutunyonya tuu na kutuburuza sisi walala hoi na kunufaisha matumbo ya wakuu wa nchi hii na mabwana zao majuuu
Ni kweli Morogoro kuweni na msimamo. Wizi tu, hizi mashine sio lolote ni ukandamizaji tu wa wanyonge. Zingekuwa dala 100 afadhali. Ni kikwazo tosha.
Post a Comment