ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, December 22, 2013

ALICHOSEMA MINZIRO BAADA YA KIPIGO CHA 3-1

 
Kocha msaidizi wa mabingwa hao, Fred Felix Minziro amesema wakati wa kupanga timu kwa mazoea sasa umekwisha na wachezaji wanaocheza soka la mdomoni hawana nafasi katika timu yao. Minziro alisema hayo wakati akizungumzia timu yake huku akiponda kikosi cha kwanza na kukimwagia sifa kikosi kilichoingia na kuwazuia Simba kufunga mabao zaidi na wao kupata bao moja. Alisema kuwa haikuwa Yanga anayoifahamu katika mchezo huo huku wachezaji wake, Hamis Kiiza,
Didier Kavumbagu na Athuman Idd wakicheza chini ya kiwango na kuwapa mwanya Simba kutawala
muda mwingi hasa eneo la kiungo. "Nimemwambia Kiiza na wenzake, soka la mdomoni kwa sasa halina nafasi, wengine wameshindwa kufanya kile tulichowafundisha na kuwaagiza, walichokifanya ni
madudu na kushindwa kutufadhaisha," alisema Minziro. 

Alisema kuwa amefuraishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji kama Hassan Dilunga, Simon Msuva, Juma Abdul, Jerryson Tegete na wachezaji walioanza, Frank Domayo, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima kwa kuonyesha kuwa wanaweza. "Angalia Okwi (Emmanuel), ameingia na kufanya vitu vikubwa, ameonyesha thamani yake, lakini awali, ilikuwa tofauti, Ngassa anapewa mpira, anajitahidi kuwahi, lakini hakuna mtu wa kumsaidia ndani ya mabeki watano wa Simba, haya hayakuwa mafundisho kwetu," alisema. Kuhusiana na Kaseja, Minziro alisema
kuwa ni vigumu kwa kipa kufanyakazi za ziada baada ya mabeki kupitwa na huwezi
kumlaumu, labda kwa bao la tatu ambalo limetokana na uzembe. 

2 comments:

Anonymous said...

Daa makoch muwe makin msiang wachezaj kwa majin

Anonymous said...

Makoch mna boa