ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 6, 2013

MAONI YA BASALAMA NA KIFO CHA NELSON MANDELA

Dunia ni nyumba ya kupoteza na kusahau kilichopoteza. Imekuwa ikipoteza wengi wenye historia pana zenye kubeba mengi. Wingu la kumpoteza Nelson Mandela ni zito na lenye kugusa watu wa aina zote.
Pamoja ya kuwa tunajua tukio hili linakuja, lakini hakuna aliyeweza kujitayarisha wala kuamini kama ni lenye kutokea kweli. Kuondoka kwa Madiba ni muamsho mkubwa kwa watu wa aina zote.
Madiba ni mwanaharakati aliyeweza kukubalika katika watu wenye mifumo yote, sio ya kidemokrasia wala ubepari waliweza kumkana au kudai ni wao peke yao, na kumuangalia kama kioo cha karne yetu.
Dunia inapoteza,lakini hakika upotezaji huu ni mkubwa na wa aina yake. Madiba ameacha mafundisho ambayo yanahimili kishindo chochote na bila shaka yakiigwa, dunia haina budi ila Amani ya kweli. Na ugumu wa njia aliyopita ndio iliyompelekea Madiba kuwa kioo cha dunia.
Miaka 20 iliyopita nilibahatika kumuona Nelson Mandela alipokuja Tanzania,.  Dunia! Hakika imepoteza.
Dunia imesimama kwa kumtambua Madiba, kila kona inamzungumzia mazuri yake na yenye kujitosheleza, na kila nchi inaomboleza kivyake. Kiongozi aliyeweza kutenda zaidi na zaidi ya aliyoyasema.
Kila mmoja wetu ana la kujifunza kutoka kwa Mwanaharakati huyu, na bila shaka hiyo ndio njia pekee ya kumuenzi Madiba.
Madiba, nenda kapumzike, nenda kapumzike. Tutakukumbuka daima.

No comments: