Sure Boy atakosa mechi hiyo kutokana na kuwa na kadi nyekundu aliyoipata katika mechi ya juzi dhidi Uganda.
Ulimwengu alisema anaumwa nyama za paja wakati Ngasa aliyefunga mabao mawili juzi ameumia kifundo cha mguu 'enka'.
Akizungumza na gazeti hili, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kim Poulsen, alisema, hana hofu na wachezaji hao na kwamba siku hizi mbili (jana Jumapili na leo Jumatatu) atazitumia kujipanga upya.
Kim alisema amekuja na wachezaji wenye uwezo na kila mmoja atampangia jukumu lake kutokana na nafasi atakayompanga.
Alieleza kuwa, anajua mechi ya kesho dhidi ya wenyeji pia itakuwa na ushindani, lakini juhudi za wachezaji wake ndizo zitafanikisha Kilimanjaro Stars ipate matokeo mazuri.
"Kila mchezo unajipanga kutokana na mazingira ulionayo, tunatulia leo na kesho, halafu tutajua tuikabili vipi Kenya," aliongeza Kim ambaye aliutazama mchezo kati ya Kenya na Rwanda .
Kilimanjaro Stars na Kenya zitacheza nusu fainali ya kwanza na mshindi atafuzu kucheza fainali ya michuano hiyo ya kila mwaka itakayofanyika Alhamisi kwenye Uwanja wa Nyayo, jijini Nairobi.
Mshindi kati ya timu hizo atavaana na timu itakayoshinda kati ya Zambia (Chipolopolo) na Sudan ambazo jana zilizitoa Bunrundi na Ethiopia.
Hata hivyo, Poulsen, alisema baada ya kuitoa Uganda, anaamini timu yake sasa ni tishio katika mashindano ya Kombe la Chalenji na hakuna wakuweza kuwatisha.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment