ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 27, 2013

RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI

 Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal akimlaki Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Kuwasili nchini akitokea jijini New York Marekani ambapo alikwenda kwa ukaguzi wa kawaida wa afya yake.Akiwa nachini Marekani Rais Kikwete alialikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban ki Moon nakufanya naye mazungumzo kuhusu ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika ulinzi wa Amani katika nchi mbalimbali.
Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal akizungumza na Rais Dkt.Jakaya Kikwete  Mrisho mara baada ya kumlaki muda mfupi baada ya Kuwasili nchini  akitokea jijini New York Marekani ambapo alikwenda kwa ukaguzi wa kawaida wa afya yake nchini Marekani. Rais Kikwete alialikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban ki Moon na kufanya naye mazungumzo kuhusu ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika ulinzi wa Amani katika nchi mbalimbali.Picha na Freddy Maro

1 comment:

Anonymous said...

Karibu JK, next trip where?