Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga,Abdallah Bin Kleb.
Klabu ya Yanga itatema yosso wake wote kutoka timu A katika jitihada zake za kujidhatiti kwa ajili ya kufanya vizuri katika duru la pili la ligi kuu ya Bara na michuano ya kimataifa mwakani.
Akizungumza na Nipashe jijini jana, mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Bin Kleb alisema kuwa klabu yake bado ina nafasi mbili za kusajili wachezaji katika dirisha dogo hili.
Ufafanuzi huo wa Bin Kleb umekuja kufuatia wasiwasi kwamba timu hiyo imezidisha idadi ya wachezaji ambao wanaruhusiwa katika usajili mdogo baada ya kuanza msimu ikiwa na 29 na kuongeza wawili hivi karibuni.
Bin Kleb alisema katika orodha ya wachezaji 29 waliowasajili kabla ya kuanza kwa ligi Septemba, watatu waliwapandisha kutoka kikosi cha U-20.
Hivyo Bin Kleb alisema kamati yake inaendelea kuimarisha kikosi cha timu hiyo kwa maelekezo ya kocha Ernest Brandts kujaza nafasi mbili zilizobaki baada ya kuwachukua Juma Kaseja na Hamisi Dilunga mapema mwezi huu.
"Wengi wanajua sisi tumebakisha nafasi moja tu ya usajili, pamoja na kuwasajili Dilunga na Kaseja bado tuna nafasi nyingine mbili za kuongeza wachezaji ili kufikisha idadi ya wachezaji 30 kwa sababu wachezaji watatu ni wa timu ya vijana," alisema Bin Kleb.
Aliwataja wachezaji vijana waliopandishwa timu kubwa kuwa ni Bakari Masud, Issa Ngawe na Idrissa Rashid 'Messi'.
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura alisema ni kweli Yanga ina nafasi mbili zaidi za usajili mdogo kwa sababu wachezaji wa U-20 hawahesabiwi kwenye kikosi cha wachezaji wakubwa.
"Hapa ni suala la kikanuni tu... wachezaji vijana kwa maana wale wenye umri wa chini ya miaka 20 waliopandishwa timu kubwa hawahesabiwi kwenye timu ya kubwa," alisema Wambura.
"Hivyo kama wao wanao watatu ni wazi kwamba wana nafasi nyingine ya usajili."
Yanga inaendelea kusaka wachezaji ili kuimarisha kikosi kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Bara na Ligi ya Klabu Bingwa Afrika baadaye Januari, na Kombe la Kagame la Afrika Mashariki na Kati la katikati ya mwaka ujao.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya usajili walikwenda Kenya kwenye mashindano ya Kombe la Chalenji la Afrika Mashariki na Kati wiki hii kwa lengo la kusaka mshambuliaji mmoja wa kimataifa.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment