ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 7, 2014

BALOZI MWANAIDI MAAJAR AWAPA POLE WAZAZI WA MPENDWA WETU ZAINAB BUZOHERA NYUMBANI KWAO UKONGA BANANA

 Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Balozi Mwanaidi Maajar akiongea na mama wa marehemu wa Zainab Buzohera alipokwenda kuwapa pole wanafamilia wa mpendwa wetu nyumbani kwao Ukonga Banana, Dar es Salaam Tanzania leo Jumanne Jan 7, 2014.
 Balozi Mwanaidi Maajar akiongea na Baba wa marehemu leo Jumanne Jan 7, 2014 alipokuwa amekwenda nyumbani kwa wafiwa Ukonga Banana kutoa mkono wa pole kwa wazazi wa mpendwa wetu Zainab Buzohera aliyefariki siku ya Jumamosi Jan 4, 2014 katika hospitali ya Doctor's Community iliyopo Lanham, Maryland nchini Marekani.
 Kushoto ni Lovenes Mamuya mmoja wa marafiki wa marehemu anaishi DMV nchini Marekani akiwa pamoja na Balozi Mwanaidi Maajar (watatu toka kushoto) wakiwa nyumbani kwa familia ya mpendwa wetu Zainab Buzohera Ukonga Banana, Dar es Salaam, Tanzania walipokwenda kuwapa pole wazazi na ndugu, jamaa na marafiki wa karibu na marehemu.

 Balozi Manaidi Maajar akiongea na Baba mzazi wa marehemu nyumbani kwao Ukonga Banana leo Jumanne Jan 7, 2014 aliopokuwa amekwenda kutoa mkono wa pole kwa wazazi na familia ya mpendwa wetu Zainab Buzohera aliyefariki siku ya Jumamosi Jan 4, 2014 katika hospitali ya Doctor's Community.
 Wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki wakiwa msibani Ukonga Banana

7 comments:

Anonymous said...

Jamani huyu balozi ana roho ya ubinadamu jamani mungu amuongezee yani amekwenda kutoa pole.Mama ubarkiwe sana sana wewe ni kiongozi hakika mama unastahili sifa

Anonymous said...

Mama ilove you so much ubarikiwe na mungu wa mbinguni

Anonymous said...

She is real!! ona hata alivyovyaa, wanawake huenda hivyo kwenye misiba. Good on you Sinare.

This is the one who should be a Minister.

Anonymous said...

Si kiongozi tu huyu ni mzazi,yaani ni mama she knows what those Parents are goin through,thanks mama balozi

Anonymous said...

Mfano wako ni wakuigwa na viongozi wengine. That's very nice of you. Mama na baba Zainab, poleni sana. Kazi ya Mungu.

Anonymous said...

Natoa Pole nyingi sana kwa Wazazi, ndungu na jamaa wote wa marehemu mpendwa wetu Dada Zainab. Tupo nanyi katika kipindi hiki kigumu. Rest in Peace sister Zainab.

Anonymous said...

Alikuwa anaumwa nini? RIP