ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 6, 2014

HAPA NA PALE YA VIJIMAMBO KUTOKANA NA HALI HEWA MWANZO WA MWAKA 2014 ILIVYOKUWA KATIKA MIJI YA CHICAGO, MICHIGAN NA MINNESOTA JUMATATU

Vikwangua hanga vya mji wa Chicago ulikumbwa na ukungu mkubwa uliosababisha hadi ndege kusimamisha shughuli zake. Hali hii ilikuwa imesababisha kuwepo kwa baridi kali sana tempreratures kuwa chini ya 0. Wanafunzi katika shule za serikali waliambiwa wasiende shule kwani hali ya baridi ilikuwa mbaya sana.
Hii ni katika Jimbo la Minnesota mto maji yalikauka na kuwa jiwe baada ya baridi, huyu bwana akaamua kuchukua skis zake na kutembea juu ya mto huo kama vile barabara ya kaiwaida bila madhara yeyote. 
Usije dhania kuwa hapa ni katika sayari ya (MARS) hapana ni mto huu umeganda kutokana na baridi hadi jamaa anakatiza shortcut bila hata kuzama. Baridi la huko Jimbo la Minnesota ni habari nyingine, hii ni jumatatu ya tarehe 6 hakuna cha kwenda shule wala kazini.
Pata hisia wewe mwenzangu na mi ndiyo umeingia tu kutoka barabara ya 14 pale Tanga na umevaa kata mikono yako ukatupwa pahala hapa si utamwita Mungu majina yote. Hii ilikuwa Indianapolis jumatatu hii temperatures chini ya 0, kazi hiyo.
Jamaa alivunja rekodi kwa kujikinga na baridi maana hata macho uwezi kuona baridi mbaya saana.
Kazi ya siku ya huyu dereva ndiyo iliishia hapa hapa baada ya lori lake kushindwa kuendelea na safari na kukwama kabisa kutokana na theluji kuwa nyingi barabarani.

No comments: