Mume wa marehemu Dullah na mdogo wa marehemu Ngalu Buzohera wakiwa kwenye harambee ya kuchangisha fedha za kusaidia kusafirisha mwili wa mpendwa wetu marehemu Zainab Buzohera aliyefariki Jumamosi Jan 4, 2014 saa 2 usiku (8pm ET) WanaDMV walijumuika katika harambee iliyofanyika Bladensburg, Maryland na kuchangisha $22,938 kiasi kilichokuwa kinatakiwa ni $15,000 hii inamaanisha wanaDMV wanapoamua hufanya kweli shukurani kwa wote walioshiriki harambee hii kwa njia moja au nyingine lengo ni kufanikisha na Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema tunashukuru kwa kutuwezesha kufanikiwa harambee hii ya mpendwa wetu Zainab Buzohera. WanaDMV tunawashukuru wenzetu wa New York waliofika kwenye harambee hii kuja kusaidia kutimiza malengo.
Dada wa marehemu Jasmine Bernett akiongea kwa niaba ya familia ya Buzohera huku akiwa amejawa na uso wa huzuni aliwashukuru wote waliofika kwani lengo ni kusaidia kuchangia ili mwili wa marehemu Zainab uweze kusafirishwa nyumbani Tanzania kwa mazishi na matarajio ni kusafirisha siku ya Jumatano na kisomo kinatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne jioni mahali patatangazwa baadae.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn Idd Sandaly akielezea utaratibu wa harambee.
Dada Tuma akielezea utaratibu wa mnada utakavyokuwa.
washika mahesabu wakijiweka sawa kabla ya harambee kuanza.
Watanzania waliofiika kwenye harambee wakitoa michango yao kabla ya harambee haijaanza/
Michango ikiendelea kabla ya harambee.
Timu ya New York ikitoa mchango wake.
Dada Tuma akiendesha mnada.
Umati wa Watanzania waliokuja kwenye harambee.
Watanzania kutoka New York katika picha ya pamoja.
Kutoka kushoto ni Yunus, Bob Miano, Mmiliki wa Vizion One Abdallah Kitwara na Albert Mateso wakiwa kwenye harambee.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
9 comments:
DMV wanavulia kofia - nyie ni watu haswa, anyway poleni kwa msiba na endeleeni na utu wenu. Mungu awajalie
DMV wanavulia kofia - nyie ni watu haswa, anyway poleni kwa msiba na endeleeni na utu wenu. Mungu awajalie
WATANZANIA WA DMV KWELI MNA UMOJA SANA NA MUNGU AWAZIDISHIE, KWANI MNAONEKANA JINSI GANI KTK SHIDA MNAVYOKUWA KITU KIMOJA NA KWELI HUKU TULIPO NI MBALI NA TATIZO HATA SIKU MOJA MTU ALIOMBI LINATOKEA BILA MTU KUJIANDAA.
MIOYO YENU YA UPENDO NAKUTOA KWA MOYO MSICHOKE NANYI MUNGU ATAWALIPA,KWANI HAKUNA AJUAE LA KESHO WALA LA BAADAE ZAIDI YA MUNGU NDIO ANAKUJUA WEWE UTOKAPO NA UINGIAPO NA UAMKAPO NA ULALAPO....RIP ZAI.
miji mingine igeni mifano huku mbali tulipo kujaliana zaidi wakati wa matatizo ndio kilicho kikubwa kwa mwanadamu tusiishi kwakuangalia uzito au wepesi wa mtu.
Mapenzi yenu hayana mfano. Umoja wenu niwakupigiwa mfano.
Pole za dhati kwa wafiwa. Mola muweza amsamehe makosa yake na amuweke kwenye pepo yake takatifu. Amin.
Haji Rajab Haji. Bellevue, Washington.
kweli wana DMV ni Mungu tu anayewajalia huo moyo wa kutoka mwenzenu anapopata matatizo na mtazidishiwa mara sabini.Unaonekana umoja wenu kwenye tatizo ni mko mbele na msichoke,na mnaonekana mnaitikia wito kweli kweli kwani tatizo linatokea wanaume wanaambiwa walete vinywaji na wanawake vyakula na mnaitikia kwa furaha kwa moyo mmoja,sina wakuwafananisha na nyie ila inabidi na miji mingine tuige mfano kwani huku tulipo ni mbali na tatizo haliombwi hata siku moja ila linakuja kama mwizi.
miji mingine mtu akipata tatizo badala yakusaidia kwa moyo mmoja yanaanza kwanza majungu na sababu zisizo na msingi,jamani kwanini tusiwe na moyo wakusaidia kutoka rahoni kama wenzetu bila kutanguliza kwanza majungu?tutabalikiwa vp wapendwa?jamani tujifunze kuwa na umoja kama wenzetu wa DMV si kutanguliza majungu ktk tatizo la mwenzako hakupenda limtokee na hakuna mtu anayeomba tatizo limtokee.
I CAN STAND TALL AND SAY WITH A PRIDE THAT I'M TANZANIAN WHO HAPPEN TO LIVE WITHIN A GREAT COMMUNITY OF DMV. PAMOJA NA MAPUNGUFU YETU YA HAPA NA PALE BUT WE ARE A WORKING PROGRESS. TUENDELEE KUSHIKAMANA. #LOVE U ALL#
mapungufu kwa mwanadamu yapo sana ila kwa kushikamana ktk matatizo ndio jambo kubwa kwa mwanadamu,DMV kuweni na moyo huo huo nadhani na miji mingine watajifunza toka kwenu,kwanza kikubwa mnaonekana tatizo likimpata mwenzenu taarifa ikiwafikia mnajali sana kuuitikia wito na ndio inavyotakiwa si kuanza majungu huyu hivi huyu vile pia Mungu hapendi roho za majungu.
Post a Comment