ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, January 4, 2014

MNIGERIA ANASWA NA SEMBE UWANJA WA NDEGE BONGO LIVE!!

RAIA wa Nigeria, Okwubili Agu (40), amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) akiwa na pipi 71 za dawa za kulevya aina ya heroin, zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 54, alizokuwa amezimeza tumboni.
Kamanda wa Polisi wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya nchini, Godfrey Nzowa alisema jana kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi majira ya saa 4 usiku katika uwanja huo. Nzowa alisema kuwa mtuhumiwa huyo 
alikamatwa na Kikosi Kazi kinachofanya kazi katika Uwanja huo, akiwa katika harakati za kusafiri na ndege ya KLM kwenda Amsterdam, Uholanzi.
Credit:HabariLeo

1 comment:

Anonymous said...

Ngoja niwanong'oneze wameza dawa
Ile x ray tuayopitaga airport, ina uwezo wa kuangalia kama kuna kitu kisicho kawaida tumboni. Mtakamatwa tu miaka hii.