Moshi ukiwa umetanda angani baada ya nyumba ya mmiliki aliyefahamika kwa jina la Abdallah Mkambala yenye namba 91T kuungua moto katika mtaa wa Uhuru na kuharlibu mali mbalimbali zilizokuwemo ndani kwa kuteketea kwa moto majira ya saa 11 jioni Manispaa ya Morogoro jana, hata hivyo chanzo cha moto huo hakijaweza kufahamika mara moja.
Raia wema wakisaidia kuzima moto.
Askari akihakikisha utulivu unakuwepo kutokana na majanga kama hayo watu wenye tabia za udokozi hawakosekani ili rahisi kuwadhibiti.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Pascal Mwakambungu kushoto akitoa maelekeza juu ya kuimalisha ulinzi eneo hilo.
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Morogoro Bonifance Mbao na Mhe Hassan Malingo wakiwa eneo la tukio.
Wasamalia wema wakisaidia kuvuta mpira wenye maji ili wafanyakazi wa Zimamoto waweze kuzima moto
Uokoaji wa mali huku mfanyakazi wa zimamoto akimalizia kuzima moto huo uliodumu kwa zaidi ya daka 34.
PICHA/MTANDA BLOG
No comments:
Post a Comment