Kwa siku mbili zijazo, Wamisri watajua ikiwa watakuwa na katiba mpya au ikiwa rasimu ya katiba inayopigiwa kura haitaidhinishwa.
Baadhi walihisi huo ndio ulikuwa mwisho wa siasa mbaya lakini baadaye rais aliyechaguliwa kihalali Mohammed Morsi, aliondolewa mamlakani na jeshi

Morsi alikuwa mwanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood ambalo ikiwa katiba hii itapitishwa ndio itakuwa mwisho wake. Chini ya Katiba mpya Vyama haviwezi kuundwa kwa misingi ya kidini, kabila, jinsia na kijiografia. Bila shaka itakuwa pigo kubwa kwa vuguvugu la Muslim Brotherhood

Misri pia imekuwa ikikumbwa na hali mbaya ya usalama. Mashambulizi ya kulipiza kisasi na ya kuvizia yakiwa jambo la kawaida. Chini ya katiba hii waziri wa ulinzi sharti awe mwanajeshi kama hali ilivyo sasa.

Ulsama ulidhibitiwa kote nchini humo kwa hofu ya mashambulizi

Wake kwa waume, wazee kwa vijana wote walijitokeza kwa hamu ya kuipatia Misri mustakabali mwema wa kisiasa
Wake kwa waume, wazee kwa vijana wote walijitokeza kwa hamu ya kuipatia Misri mustakabali mwema wa kisiasa

Kwa siku mbili zijazo, Wamisri watajua ikiwa watakuwa na katiba mpya au ikiwa rasimu ya katiba inayopigiwa kura haitaidhinishwa.

No comments:
Post a Comment