ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 16, 2014

RAIS KIKWETE AWAAPISHA BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI MALAYSIA NA KAMISHNA WA TUME YA USULUHISHI

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana asubuhi amewaapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia na Kamishna wa Tume ya usuluhishi na Uamuzi.Walioapishwa leo katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam ni Dkt. Aziz Ponary Mlima anayekuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia na Bwana Jafari Omari  anayekuwa Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi. Pichani ni Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam jana Jan 15, 2014.
 Kamishna wa Tume ya usuluhishi na uamuzi Bwana Jafari Omari akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam jana asubuhi Jan 15, 2014.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wateule aliowaapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kushoto ni Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Bwana Jafari Omari na kulia ni Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt.Aziz Ponary Mlima. Picha na Freddy Maro.

No comments: