
Mchezaji wa Tanzania, Shadya Kitenge akirudisha mpira kwa mpinzani wake, Vannesa Egesa wa Kenya wakati wa mashindano ya vijana kwa nchi za Afrika Mashariki, yanayoendelea kwenye Viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam jana. Shadya alifungwa 6-1, 6-0. Picha na Joseph Zablon
Dar es salam. Tanzania jana ilianza vizuri mashindano ya vijana ya Afrika Mashariki na Kati baada ya wachezaji wake Mernad Frank na , Emmanuel Mallay kushinda katika michezo yao ya jana kwenye Viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam.
Chipukizi wa Tanzania, Mernad Frank alimshinda kirahisi Kigotho Oliver wa Kenya kwa 6-0, 6-1, huku Emmanuel Mallay wa Tanzania akimbwaga Hassan Maouland wa Comoro kwa 6-0, 6-0.
Katika mchezo huo Mallay hakupoteza mipira yote aliyoanzisha kwa kupiga mipira kwa kasi katika kona za uwanja iliyomfanya Maouland apigwe na butwa muda wote.
Mallay alisema alicheza hivyo na kumshinda mpinzani wake mapema ili asichoke na kujiandaa na michezo migumu itakayokuja.
Katika mchezo mwingine, Ibrahimu Sadick wa Tanzania alimshinda Molla Nehma kutoka Ethiopia kwa 6-2 na 6-1, naye Salehe Aahil kutoka Kenya alimbwaga Hassan Hamisi wa Tanzania kwa seti 6-2, 6-4.
Pia Tuyshime Fabrice kutoka Rwanda alimshinda Salehe Rashid kutoka Tanzania kwa 6-2, 5-7 na 6-0 katika mchezo uliokuwa na mvutano mkubwa.
Katika mchezo mwingine, Deme Zekaria kutoka Ethiopia alimshinda Hamza Ali wa Tanzania kwa 6-4, 6-1 katika mchezo wa kuvutia.
Mashindano hayo yanashirikisha wachezaji vijana kutoka nchi za Burundi, Comoro, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Shelisheli, Sudan na wenyeji Tanzania.
Mwanachi
No comments:
Post a Comment