
KABLA ya yote natanguliza shukrani zangu kwa mwenye miliki ya mbingu na dunia kwa kuweza kutuamsha salama siku ya leo ikiwa ametuwezesha kuvuka upande wa pili wa mwaka ambao wenzetu wengi hawakufanikiwa kuiona siku ya leo ya Mwaka 2014. Kila mmoja ana kila sababu ya kumshukuru Muumba kwa mapenzi aliyompa ya umri na afya njema.
Kona hii kama ada kunyoosha tabia za watu wanaojifanya wameshindwa kunyooshwa na wazazi wao. Huu dada ni muarobaini unatibu magonjwa zaidi ya elfu moja, lazima la kwako itakuwemo. Kwangu si lazima nikufikie, kuona kwako ndiko kupona kwako.
Sitaki kubwabwaja sana na kuwanyima uhondo japo kwa wengine huwa subiri ambayo akiimeza lazima afumbe macho na akifumbua keshapona huyo. Jamani mashostito wangu ambao hamna wapenzi najua jinsi gani unavyoitafuta pesa kwa nguvu nyingi na siku moja mnataka kupumzika na kula raha.
Najua mnapenda kutumia pesa zenu kwa kutafuta mwanaume ambaye atakuwa chini ya miliki yenu kwa kumiliki haki zake zote kwa vile hupendi karaha unataka kula raha baada ya kuzitafuta kwa muda mrefu au mjane ambaye bado damu inachemka na anataka kuwa na mtu mwenye staha zake.
Furaha yenu ni kumtafuta mtu anayejiheshimu hata akiwa amemzidi umri kikubwa heshima. Lakini baadhi yenu tumekuwa wakitafuta vijana wa kustarehe zao wakati huohuo tuna bwana mwingine ambaye ndiye anayeingiza kipato.
Kwa vile kijana uliyenaye umemmiliki kwa asilimia kubwa unakuwa humheshimu kwa vile kitu unampa na kusahau kitu muhimu kuliko vyote hapati kwako nacho ni heshima.
Wengine hudiliki kuwatukana wapenzi wao kwa vile tu wana pesa ambayo huamini ndiyo inayomuweka kwako na kusahau utu ni bora kuliko mali.
Hapa ndipo paliponifanya nizungumze na ninyi mashostito wangu mwanzo wa mwaka. Jamani kuwa na pesa bado hakuondoi uanamke wetu na kufikia hatua ya kuwageuza wanaume tunaowamiliki kuwa wanawake na sisi ndiyo wanaume.
Shoga hata siku moja masikio hayazidi kichwa, siku zote bado tutatangulia chini kwa vile ndiyo maumbile tuliyoumbiwa. Hivyo basi uanamke wetu hautabadilika kwa vile tuna pesa au tuna uwezo wa kumiliki mwanaume.
Hebu tuuheshimu uanamke wetu hata tunapozungumza na wapenzi wetu tunao wamilimiki turudi kwenye uanamke wetu hata tunapozungumza nao turudi chini siyo kuwapanda juu kwa vile tuna fedha.
Kwa mtindo huo tutakuwa mung’unya kuharibikia ukubwani, kwani ni aibu mtu mzima kuwa mama huruma kwa kubadili wanaume.
Jamani kama hukutosheka katika ujana wao utatosheka uzeeni? Hebu basi kama kweli tumeamua kumtafuta mtu ili tutulie naye basi tunatakiwa kujiheshimu na kumuheshimu uliyemtafuta kwa wewe kuwa mwanamke na yeye mwanaume.
Namalizia kwa kusema Mungu alituumba kuwa chini ya wanaume tuna haki ya kujitetea pale panapostahili hata kudai talaka lakini si kuwadharau wanaume kwa vile tuna uwezo mkubwa wa kifedha na kukua masikio kuzidi kichwa.
Sifa ya mwanamke ni unyenyekevu kwa kuamini utu ni bora kuliko mali. Mali inaisha lakini utu wa mtu hauishi.
Napenda kumalizia kwa kuwatakia heri ya mwaka 2014, Mungu atupe kila la heri na kutuepusha kila la shari.
Ni mimi Anti Nasra Shangingi Mstaafu.
GPL
1 comment:
makala nzuri na umepasua ukweli lakini aliyeandika ni mwanamme na kila leo ndo haya hayo ya kumuona mwanamke duni ni kweli kuna wanawake wenzangu wako hivi lakini wanaume ndo wamezidi zaidi na wakiwa na pesa kila leo na kina kona vimada etc so what about that au tena ndo maskio hayazidi kichwa lakini umesahau masikio yana nguvu kubwa kuliko kichwa hata juu ya udogo wake
ni kweli heshima kitu cha bure na lazima tuheshimiyane lakini kwa pande zote mbili siyo kila leo mwanamke awe mnyonge kisa mwanamke unajua kwa nini wanawake wanafanya hivyo wakiwa na pesa kwa sababu wanaume wamewafanyia hivyo na kuwanyanyasa sana ni jambo la ki psychologia so tuelimishane vizuri jamani siyo MADOIDO YA SIKIO HAKIZIDI KICHWA.
Kheri ya mwaka mpya wana blog wote
Post a Comment