ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 8, 2014

YAHUSU COMMENT KWENYE VIJIMAMBO

Habari za leo wadau wa Vijimambo sisi hatujambo nimatuamini yetu wewe na familia yako ni wazima wa afya na mumeuanza mwaka mpya kwa nguvu zote. Nia na madhumuni ya waraka huu nikutaka kuwekana sawa kuhusiana na Comment (maoni) ya wadau wanayotoa kwenye Blog hii yenu ya Vijimambo. kwa mfano leo kuna mdau alituma maoni yake na hayakutolewa kwa muda ule aliokuwa ametoa na baadae akaghafirika na kuja juu akimshutumu Dj luke kwanini anabania Comment, kwanza kabisa mdau timu Vijimambo tunaomba radhi kwa kuchelewa kutoa comment yako na kusababisha na wewe kupata hasira na kuandika comment zingine zilizokuwa na lugha ya ukali.

Kuna mambo kadhaa naomba nikueleshe ambayo yanaweza kuwa sababu ya comment yako kuchelewa kutolewa hewani.

1. Waendeshaji wa Blog yako wanaendesha maisha yao kwa kupiga box kama watu wengine waliopo ughaibuni wanavyoendesha maisha yao ya kujipatia riziki kwa mtindo huo ili waweze kujikwamua na gharama au kupooza ukali wa maisha ya majuu.

2. Aliyepewa jukumu la kuchuja Comment kwenye Blog yako ni Dj Luke peke yake na kama ujuavyo anamajukumu mengi ya kupiga box na kuihudumia jamii inayomzunguka ukiwemo wewe mwenyewe bila kujali kabila, rangi, jinsia, umri, cheo, dini au itikadi za vyama. Timu ya Vijimambo inatambua na kuamini watu wote ni sawa wanastahili huduma sawa bila upendeleo ndio maana Blog yako haichagui wala haibagui mtu kwani wote wanastahili kupata huduma sawa. 

3. Timu ya Vijimambo inatambua kwamba Mdau ndiye Boss wa Blog hii na sisi ni waendeshaji tu bila nyinyi kazi yetu ya uendeshaji isingekuwepo.

4. Timu ya Vijimambo inakuomba radhi tena kwa usumbufu iliokusababishia na si kosa lako ni kwa sababu hatukukueleza mapema kwamba hatuendeshi Blog hii saa 24, siku saba kwa wiki japo tungependelea iwe hivyo lakini kama tulivyoelezea hapo juu muda mwingi tunapiga Box hatupo kwenye mtandao muda wote kwa hiyo tuwiye radhi mdau tunakuomba uvute subira Comment yako itatoka.

Baada ya kusema hayo nadhani Mdau utakua umetuelewa na tunaomba tuishie hapa kwa leo.

Asante, Timu Vijimambo

2 comments:

Anonymous said...

Hii pia inachekesha kama sio kuchanganya zaidi.Imeeleweka mnapiga box,na comment hutolewa kulingana na muda habari iliotoka,sasa ikiwa Dj liuke hana muda wa kuruhusu comment kwa muda muafaka inawezekana comment hiyo isisomwe na yeyote kwani habari husika itakuwa page ya nyuma zaidi,hivyo kufanya comment husika kukosa maana kabisa.Ikiwa hana muda basi acheni comment box iwe huru yaani isichujwe ili kuirusha itoke ilivyo kwa muda iliyotumwa na muhusika ,kwani lengo la kutoa comment pia ni kutoa angalizo au ujumbe kwa mujibu wa habari husika,Sasa ikiwa hakuna muda wa kuchambua ipi nzuri na ipi mbaya ,basi ziruhusiwe hivyo hivyo.kwani zinamdhuru nani?! msomaji au mtoa habari?? weka zilivyo kwani hata habari kuna habari huwa zinawekwa hapa hazitufurahishi sote.kuna zinao walenga na hufurahishwa nazo na kunawanao gadhabika na habari hizo.Hivyo basi uwanja huu usiwe na upendeleo kwa moderator tu,kama navyochukizwa na habari fulani na kufurahishwa na nyingine vivyo hivyo kwa wasomaji.na kwakuwa huwezi kumfurahisha kila mtu,basi jamvi limeisha tandikwa usichague wakaaji,tupo wenye miguu michafu au suruari chafu pia tunataka kukaa juu ya jamvi pia, na wale wasafi wakiona hapawafai watatafuta jamvi lao, ilimradi sote tushiriki humu ndani.lakini kuamua muda wa kurusha maoni ya mtu au kutorusha kabisa kwasababu ajuazo moderator kwa kisingizio cha muda,hiyo siyo haki.hatuwezi kila mtu kuwa na blog,ila kama ulianzisha kwaajili yetu acha tukosoane,usituchagulie kasoro.kama ulianzisha kwqa ajili yako basi zuia tusione kabisa unachofanya humu.Tamati,ni kukuomba moderator usitumie kizingizio cha muda kutokutoa maoni ya watu.Rusha kila kitu.harufu ya perfum na mizoga zote harufu,atachagua mnusaji anuse ipi na ipi aache,siyo wewe uwe na macho yetu,masikio yetu,midomo yetu,pua zetu na hata ngozi zetu.kila mtu awe huru kwa kila maoni na habari zitolewazo humu,nyie mnaiita hii blog yetu,basi tuachieni.sisis ndio wadau wenyewe,tatizo lenu nini.

Anonymous said...

Maneno mazuri humtoa nyoka pangoni.Nimeipenda hii.