ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 9, 2014

AROBAINI YA MPENDWA WETU ZAINAB BUZOHERA DMV LEO JUMAPILI

Zainab Buzohera enzi ya uhai wake

Dullah na familia ya Buzohera inawataarifu kisomo cha arobaini ya mpendwa wao Zainab Buzohera itakayofanyika siku ya Jumapili Feb 9, 2014 kuanzia saa 7 mchana mpaka saa 11 jioni (1pm-5pm) katika mgahawa wa Tabeer uliopo Langley Park chini ya Mirage Hall anuani ni
1401 University Blvd, 
Hyattsville, MD 20783.
Tunaomba wakina baba mchangie vinywaji na akina mama mchangie chakula ili kufanikisha siku hii ambayo ilianzia saa, siku, wiki, mwezi na siku 10 sasa

Ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzio
Kwa maelezo zaidi na maelekezo tafadhali wasiliana na 

Idd Sandaly 301 613 5165
Jabir Jongo 240 604 0574
Hidaya Mahita 240 271 7799
Nuru Mwamende- 240 603 9364
Khamisa Matope- 301 910 4634
Salma Londa- 240 330 3670
Ngalu Buzohera- 240 330 0169
Farida- 240 593 7370
Habiba -240 778 7567
Asante


8 comments:

Anonymous said...

Hebu kuweni na weledi wa lugha kidogo. Si muandike tu "Arobaini" neno Forty maana yake nini sasa?

Bwana Luka vipi hii blog yako haifanyi editing?

Anonymous said...

What is your point, mdau (anonymous #1)? With all due respect, nothing is wrong with the word "Forty". Tupo ndugu ambao tunafahamu translation ya arobaini is "forty". Hata P-7 pale bongo anajua what the term *forty" means. Yours, is an unwarranted critique! Am sure you are smarter than that. Your participation will be highly appreciated!

Anonymous said...

kweli kabisa

Anonymous said...

Kiswahili kizuri ni arobaini msiharibu laugha kwa kujifanya mnachanganya kiingereza na Kiswahili. Kama mngetaka mngeandika yote kwa kiingereza. Kwanini hampendi kuambiwa ukweli.

Anonymous said...

Anonymous #2, Cha msingi nimefarijika kuona Bw. Luka amenielewa nilichomaanisha (japo wewe umeshindwa kunieleewa) ndio maana umeona sahihisho ya neno 'Arobaini' badala ya 'Forty' kama ilivyokuwa awali.

Ukweli si kila mtu ametoka ghetto au ni mpenzi wa lugha za ghetto. Hivyo weledi wa matumizi ya lugha ni lazima uzingatiwe tena kwa viwango wakati wote na si suala kuchagua kwa mtindo wa a, b, c.

Kumbuka Blog hii inasomwa na watu wengi duniani kote. Watu wa rika, elimu na upeo aina tofauti. Tunaipenda blog yetu ya Vijimambo na tunapenda iwe ni ya 'viwango' visivyotia shaka wakati wote.

Mathalani huona kwenye blog nyinginezo unakuta bandiko (posting) limeandikwa mfano; Huyu ni Sam akisheherekea happy birthday yake ya siku ya kuzaliwa?! Unajiuliza weledi wa lugha uko wapi hapa!

Uzuri Bw.Luka ni mtu wa kujishusha, msikivu na mwepesi kushaurika. Hivyo ametambua nililomaanisha. Pole sana naona umeshindwa kunielewa. Kuna mambo katika maisha kuyaelewa inachukua muda kidogo na japo yanaweza kuonekana kama si lolote lakini kuyafamu ni muhimu sana.

Mwisho, nasema tupo pamoja kwenye kisomo cha arobaini ya mpendwa wetu.

Anonymous said...

Kumbukeni yale aliyosema Rais Mstaafu Mwinyi na akatupa darsa la utumiaji wa maneno vibaya na kupotosha jamii. Haswa kwa suala kama hili la msiba ni heshima kwa muhusika kutumia lugha sanifu ya Kiswahili or proper English

Anonymous said...

Pole wadau #1 and#4! Apparently, you made such a big deal with the term "forty'. Whining about small things is pretty awkward. What matters is our participation. Hizo risala zenu hazina faida, mtupe kapuni.

Anonymous said...

Si ukubali umechemsha yaishe? Huu ushamba wa lugha utatuisha lini? Hi I ni vijimambo blog ya waTanzania.. Waswahili sasa wewe kutuchanganyia lugha siunajidhalilisha...au ndiyo kasumba ya lugha? Kazi bado tunayo Wadanganyika :( kuna blog zaidi ya 1000 za kiingereza siupeleke maoni yako huko! Mwenye blog amejisahihisha wewe bado hutaki kukubali: (