
Mwalimu
wa madrasa ya Ali Munawar, ustaadhi Mohamed Ngulanjwa (36) wa Mbagala
Mianzini jijini Dar es Salaam, ameuawa baada ya kumchinja mwanafunzi
wake.
Kaimu
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Jonathan Shana, akizungumzia mauaji
hayo , alisema tukio hilo la kinyama, lilishuhudiwa na wananchi
waliomuua ustadhi huyo.
Alisema baada ya mwalimu kumuua mwanafunzi wake wa kiume alichukua kisu alichotumia pamoja na msahafu na kukimbia.
"Ilidaiwa
kuwa alimchukua mtoto huyo , kumlaza chini kisha kumchinja kwa
kutenganisha kichwa na kiwiliwili na kutelekeza vipande vya mwili wake
kwenye varanda," alisema Kamanda Shana.
Baada ya
mauaji hayo mtuhumiwa alianza kukimbia lakini wananchi walimvamia na
kumshambulia kwa mawe na kila silaha iliyokuwa karibu na kumuua papo
hapo.
Shana alieleza kuwa polisi walifika eneo la tukio na kuchukua maiti hizo na kuzipeleka hospitali ya Temeke.
Hata hivyo alisema jina la mtoto huyo mwenye umri kati ya miaka 10- 12 halikufahamika na polisi inaendelea na uchunguzi
3 comments:
Sasa Mh DJ Luke, hizi picha zinauhusiano gani na habari hii. Aliyechinjwa alikufa na aliyechinja alikufa. Polisi walifika kuchukua maiti zote mbili. Huyu anayechukuliwa na polisi sidhani kuwa ni maiti. Je ni huyohuyo anayelia hapo kwenye picha ya pili?
Nimeshindwa kupata uhusian wa picha na tukio la mauaji. Je huyu anaeonekana ktk picha ni mzazi wa mtoto aliyeuawa?
Tukio hili linasikitisha sana . Poleni wafiwa wa pande zote mbili.
Picha hii ni mnaigeria kamuua mkewe na yeye kahukumiwa kifo, Dj Luke usichanganye mambo sio lazima uweke picha.
Post a Comment