ANGALIA LIVE NEWS
Monday, February 10, 2014
JESHI LA AUSTRALIA LAKAMATA MADAWA YA KULEVYA PWANI YA TANZANIA-GPL
JESHI la majini la Australia limekamata na kuharibu kilo 353 za madawa ya kulevya aina ya heroin yenye thamani inayokadiriwa kuwa zaidi ya dola milioni 700 katika pwani ya Tanzania.
Askari wa meli ya HMAS Melbourne waliyagundua madawa hayo katika meli moja Jumatano iliyopita wakiwa katika shughuli za kupiga vita ugaidi na kuimarisha usalama maeneo ya baharini Mashariki ya Kati na Bahari ya Hindi.
Mkuu wa kikosi hicho, Daryl Bates, alisema hatua hiyo ilikuwa ni pigo katika kukwamisha njia za kupatikana kwa fedha zinazotumiwa na magaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
wadau mbona yale madawa ya tunayoona yanakamatwa Dar airport hatuoni wakiteketeza kama haya
mizigo ya wakubwa huko Bongo
That's a great question mdau sijawahiiiii kuona Tanzania wakiyahatibu au kuteketezaaaa madawa wanauoyakamataaa!!! Why? Mmmh !
Post a Comment