ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 8, 2014

JICHO LA VIJIMAMBO MTWARA BAADA YA WANANCHI KUANDAMANA KUPINGA GAS KUONDOKA JE NENO ( OMNIVERSARATISM) LITAFANYA KAZI YAKE

Rais wetu siku ambayo alitembelea Mtwara na kusimama sehemu ya uchimbaji gas. Sasa kazi imeshaanza baada ya serikali kutumia njia walizo weza na kuwatuliza wananchi wa Mtwara. wananchi hao walitaka kujua rasilimali yao ikiondoka wao watafaidikaje. Lakini mwisho walikubulii uchimbaji wa gas uendelea na bomba za kupitisha gas hiyo kutoka Mtwara hadi Jiji la wajanja Dar-Es-Salaam zifungwe.
Bomba zikifungwa kutoka Mtwara hadi Dar, Je wananchi wa Mtwara watafaidika na neno la (Ufanisishaji) Neno hili lina maana ya kutumia rasilimali za jamii kifaida kwa manufaa bora. kwa lugha ya kikoloni ni (Omniversaratism). Watu waliandamana kudai haki yao hadi serikali ikatumia nguvu za ziada zilizo sababisha watu 7 kupoteza maisha na wengine kuachwa majeruhi hadi sasa vilema wa maisha. Wananchi wa Mtwara wanahitaji kuona rasilimali yao inawaletea matunda ya kimaendeleo kwa kuboresha maisha ya watu wa mkoa huo. Kwa kupata Elimu bora Zahanati za kuwahudumia akina mama wajawazito na watoto, Maji salama na Barabara zitakazo pitika majira yote.
Wananchi wa Mkoa wa Mtwara waliandamana kama hivi kutaka kujua nini watakachofaidika na utajiri huo uliopo katika ardhi yao.

Je Mtoto kama huyu ataenda shule mzuri na kunywa maji salama kutokana na faida ya gas hiyo kuchimbwa kwenye ardhi yake?.
Nyumba za viongozi wa serikali zilichomwa moto kama hivi, 
Virugi kama hizi zilisababisha hospitali ya Mkomaindo kupokea maiti za watu 7 na polisi mmoja kati ya maiti hizo siku hiyo.
Vipigo kama hivi  kutoka kwa vyombo vya dola vilisababisha  vifo vya watu baada ya kuandamana na kufanya furugu kama kuchoma moto magari na majumba ya viongozi wa serikali. Mwaka sasa toka vurugu hizi kutokea January 26, 2013 huko Masasi Mtwara.
Mama kama huyu na mtoto wataweza kupata huduma bora kutokana na gas hiyo na kuacha kulala kitanda kisicho kuwa na chandaruwa na shuka zake.?
watoto watakuwa na furaha kwa kusoma wakati wamekaa kwenye madawati bila kuendelea kula vumbi kwa kukaa chini. Na watoto wengine wakibanana kama mishkaki kwenye dawati moja.?
Barabara kama hizi zitakazokuwa zinapitika wakati wote na siyo kiangazi tu. Mtwara walikuwa na haki ya kudai haki yao, kwani wanamifano kutoka mikoa mingine ya Tanzania yenye Dhahabu, Tanzanite, Gold. Na rasilimali nyingi sinazoishia kwa wajanja wanaojilimbikizia mapesa na kuwaacha Watanzania  wakiwa masikini na nchi inaendelea kuwa omba omba kila siku. Wakati mtu mmoja anamapesa ya kuweza kuikopesha serikali yenyewe na ikatengeneza daraja  la kutoka Dar hadi Unguja.

No comments: