Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) akimkabidhi zawadi Rais wa CAF, Issa Hayatou Makao Makuu ya CAF jijini Cairo, Misri.
Rais
wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) akiwa na Rais wa CAF, Issa Hayatou na
mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, Leodegar Tenga Makao Makuu ya CAF
jijini Cairo, Misri.
---
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemwahidi ushirikiano Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.
Ahadi
hiyo imetolewa juzi (Februari 21 mwaka huu) makao makuu ya CAF jijini
Cairo na Rais wa shirikisho hilo Issa Hayatou alipokutana na Rais
Malinzi aliyekwenda kujitambulisha huko.
Utambulisho
wa Rais Malinzi kwa Rais Hayatou uliongozwa na mtangulizi wake Leodegar
Tenga ambaye aliiongoza TFF kwa vipindi viwili kuanzia 2004 hadi 2013.
Tenga
ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF na Mwenyekiti wa
Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA),
alimweleza Rais Hayatou kuwa uchaguzi wa TFF ulikuwa mzuri.
Aliongeza kuwa alimkabidhi kijiti Rais Malinzi kwa maridhiano na ana imani na uongozi wake.
Rais
Hayatou alimpokea Rais Malinzi na kuahidi kuendelea kuipa Tanzania
ushirikiano hasa katika maeneo ya utawala, ufundi na kuboresha
miundombinu ya kuendeleza mpira wa miguu.
Kwa
upande wake, Rais Malinzi alisema TFF itaendelea kutoa ushirikiano wa
dhati kwa CAF ili kuhakikisha kiwango cha mpira wa miguu nchini Tanzania
kinakuwa.
Baadaye mchana, Rais Malinzi alipata chakula cha mchana pamoja na wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji ya CAF.
No comments:
Post a Comment