ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 10, 2014

SHUKRANI ZA DHATI KUTOKA KWA DULLAH KWENDA KWA NDUGU, MARAFIKI NA WATANZANIA WOTE

Mimi DULLAH,a.k.a,DULLAHYOO,DULLAHZAY.napenda kutoa shukrani za dhati kutoa moyoni mwangu kwa WATANZANIA WOOOTE waishio UNITED STATES OF AMERICA na WOOTE waishio UGHAIBUNI na WATANZANIA WOOTE waishio TANZANIA kwa mchango wenu wa HALI na MALI mlioutoa kuanzia KIFO chake hadi MAZISHI yake almarhum MKE WANGU ZAINAB HAROUN BUZOHERA,a.k.a ZAY B,ZAY HARRY,ZAY DULLAH.Bila ya nyinyi basi familia yangu ingepata MZIGO mkuuubwa sana.mwenyezi MUNGU MWINGI WA REHMA na MWENYE KUSAMEHE BASI atawalipa hapa DUNIANI na kesho AKHERA.mwenyezi mungu akuweke mahali PEMA PEPONI ZAINAB HAROUN BUZOHERA. Aaamin!

13 comments:

Anonymous said...

Sheikh Dulla tafadhali msitiri mkeo wewe ni maalim unajua fika nini dini yetu inatufundisha mambo ya kufanya kumpunguzia adhabu marehemu na kumfungulia pepo. Tujaribu kutoonyesha picha zake kaisha tangulia mbele ya haki!

Anonymous said...

Maalim Pole sana, jee huyo uliyemueka hapo ndio marehemu Bi Zay mwenyewe? Kama ndie yeye kwanza naomba hizo picha za aina hiyo usizitumie tena. Pili naomba ufahamu peopo umbali ilipo na jitihada mtu mwenyewe anatakiwa aifanye akiwa kwenye huu mgongo wa ardhi, jee Bi Zay alifanya jitihada yeyote na alikuwa anajua hivyo kuwa baada mauti maisha ni pepo au moto tu??
Sk Dullah tafuteni maisha uzunguni lakini ya wazungu waachieni wenyewe, hizo sio mila na desturi zetu as WaTZ lakini pia imani ya dini yako haipendi hayo. ALLAHUMMA FIRLAHA WARHAMHA FIL JANNNAH

Anonymous said...

Tuache u alshababy,mujahideen na uislam wa chuki.wewe unae jirga muislam, kwanza wewe ni dhehebu gani?, pili kama una dhehebu IMAMU wako ni nani?,maana kuna maimamu Kila dhehebu. Kama wewe ni SUNNI basi waache waliokua MASHIA.sababu SUNNI, HIBADHI, ANSARI SUNNI, SHIAA WOOTE wanaamin ni WAISLAM SAFI. Kwa hiyo kabla hujasoma comment naomba useme wewe ni dhehebu gani na IMAMU wako ni nani???????.

Anonymous said...

Ahsante kwa kutaka kujua dhehebu langu na Imam wangu. Kwanza napenda ufahamu Uislam ni uislam kama ulivyo mambo ya dhehebu hayakutajwa kwenye kitabu chetu kitukufu (Qur ani). Imam mkuu wa uislam ni Sayyidna Muhammad (SAW) na yeye hakutaja chochote kuhusu dhehebu wala Imam. Kwa hivyo kwa jawabu la mkato kabisa dhehebu langu ni UISLAM na IMAM wangu ni MUHAMMAD (SAW). Hayo mambo ya u alshabbaby achaneni nayo hayatapeleka popote ulimwengu huu ama kuhusu kuwa Mujaheeeden hiyo ni sifa ya muislam ni lazima tuwe hivyo ili uislam upate watetezi. Jee kuna zaidi au unataka kujua kuhusu uislam na aaakida zake?

Anonymous said...

pole sana kaka dullah,mwenyezi mungu amuondolee adhabu ya kabri almaruhuma..kaka ushauri ondoa hiyo picha ya mke wako uliyoiweka hapo msitiri mkeo kwani leo ameshafika mbele ya haki..wametakiwa wanawake wajistiri hapo hajajistir,....chondechonde kaka

Anonymous said...

kweli msitirini marehe na kumwombea, ila kuonyesha picha zake hizi sio fresh kama ile aliyovaa humuzi inawekwa sana kwenye mablog sio vema,kashatangulia mbele ya haki cha muhimu kumwombea au kuna picha nyingine nzuri tu kajisitiri mnaweza weka kama kumbukumbu,nyie watoto wa kiislamu na deni mmesoma nadhani mtanielewa, RIP Zainab Haroun

Anonymous said...

Dj Luke siku mie nikifa naomba usiweke picha yangu. ukiamua kuweka basi iwe uso tu, i am just sick and tired of people kukosoa mtu aliyetangulia mbele ya haki. as far as i can remember most of time marehemu nilizoea kumwona akiwa katinga lace wig and thats how i will always remember her. ooh mila na desturi, mila na stuli, kila mtu ana mila na desturi zake bwana mtutokee hapa na risala zenu!

Anonymous said...

mdau kweli dini yako unaijua jinsi ulivyoifafanua kweli imani unayo. ningependa ungeweka hata na jina lako. TAKBIR. DJ LUKA usiibanie hii itoe kama ilivyo

Anonymous said...

mdau hapo juu kama vile ulikuwa kichwani kwangu. mie nikidead picha yangu muweke ile niko swimming na bikini two pieces

Anonymous said...

Wewe Kama unaweza kumumbea muombee,Kama huwezi kaa kimya na Imani yako.pili jifikirie wewe lini utakufa na ujiombee mwenyewe, waacheni wafiwa wajifariji.hata dini inasema, USIMLAZIMISHE MTU KUABUDU KILE WEWE UNAABUDU. LAKUM DINU KUM WALIA DIIIN.sura ya (kul ya ayuha lkafiruuna)

Anonymous said...

kuna mtu huwa anasema sana kuhusu watu /wanawake wa kiislamu kujistiri na hata kutoonyesha hata nywele moja ktk picha,blog na hata akiwa na wageni nyumbani kwake na anaswali sala tano,guess what huyo mtu ni muongo,mchonganishi,mshirikina hakuna tena....matendo yako ndo yatakayo kustiri

Anonymous said...

mimi ningekua luka nisingeweka koment hata moja ningezichunia tu,plz luka

Anonymous said...

Bw Dullah kwanza pole,pili kuwa kama wewe achana na mawazo ya watu. Wanakwambia uache tabia za wazungu,lakini uige tabia za waharabu wakati wao wanalala kwenye majumba ya wazungu. Wewe si mtoto mdogo nakwakuwa ulimpenda mkeo,si vibaya kupost picha za kipenzi chako.hii inaonyesha nijinsi gani unammiss.