ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 9, 2014

TZ-Houston Community wafanya mdahalo wa wagombea Uongozi wa Jumuiya

Jumuiya ya Watanzania waishio katika jiji la Houston, Texas jioni ya leo imefanya mdahalo wa wagombea nyadhifa za Uenyekiti na Ukatibu mkuu wa jumuiya katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.Nafasi ya mwenyekiti inagombewa na Bw.Issa Kingu, Bw.Erasto Mvungi, Bi.Nuru Mazora na Bw.Isaiah Mgendi.Wakati nafasi ya Ukatibu inagombewa na katibu anayemaliza muda wake Bi.Leyla Kikuzi na Bw.Alfred Nkunga.

Mdahalo huo ulioandaliwa na Kamati ya Uchaguzi chini ya Mwenyekiti wake Bw.Steve Maonyesho na kuendeshwa na Bw.James Shemdoe (Moderator) ulihudhuriwa na idadi ya kuridhisha ya Watanzania waishio katika jiji hilo la Houston na kurushwa live kupitia mtandao kwa wale ambao hawakuweza kuhudhuria. Zifuatazo ni picha za tukio hilo.
Wagombea nafasi ya Mwenyekiti toka kushoto Bw.Mgendi , Bw.Mvungi na Bw.Kingu 
Moderator wa Mdahalo Bw.Shemdoe 
Bw.Alvin Lema akiuliza swali kwa moja wa wagombea 
Bw.Nkunga akiuza sera 
Wagombea 
Shughuli inaendelea 
Sehemu ya wanajumuiya wakisikiliza sera za Wagombea 
Bi.Leyla akimwaga sera 
Cameraman Bw.Fue 
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Dk.Tenende akifuatilia mdahalo kwa makini 
Maswali yakiendelea kuulizwa 
Kulikuwa na wasaa wa kufurahi pia 
Wagombea 
Bw.Mgendi akimwaga sera 
Wenye Jumuiya yao 
Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi Bw.Maonyesho 
Mwenyekiti anayemaliza muda wake Bw.Novatus Simba akichangia 
Dk.Tenende na Bw.Andrew Sanga

No comments: