ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 8, 2014

Walimu nchini waishika ‘pabaya’ Serikali

Rais wa Chama cha Walimu Tanzania, Gratian Mukoba akisisitiza jambo. Picha na Maktaba
Dar es Salaam.
Baraza la Walimu Tanzania(CWT), limesema ifikapo mwishoni wa Februari, mwaka huu, Serikali haijakamilisha madai yao yakiwamo malimbikizo ya mshahara Sh40 bilioni watatangaza mgogoro na Serikali.
Pamoja na malimbikizo ya likizo ambazo walimu hao nchini wanadai Sh21 bilioni ambazo hadi sasa hawajalipwa.
Hatua hiyo imekuja baada Serikali kuahidi CWT kuwa Februari mwaka huu, italipa madai ya walimu yanayohusiana na malimbikizo ya mshahara lakini Serikali imebadili ahadi hiyo na italipa taratibu.
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania, Gratian Mukoba alisema, kikao walichokaa Februari 4, mwaka huu, Serikali ilibadili ahadi yake na kwenda na hoja mpya kuwa madeni hayo yatalipwa taratibu kwa sababu yanahitaji kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa kuingiza madeni ili yalipwe.
Mukoba alisema vikao vya majadiliano ya mishahara vimeshafanyika kutokana na maagizo ya mahakama kuu ya Division ya Kazi ya mwaka 2012 hakuna kilichopatikana.
Alisema CWT ilikaa kuanzia Januari 27 hadi 29, mwaka huu na kuazimia kuwa, kero hizo za walimu ziwe zimepatiwa ufumbuzi hadi mwishoni mwa Februari vinginevyo chama kitangaze mgogoro na Serikali.
Alisema Serikali haikufanya maandalizi mazuri ya mfumo wa kutathmini utendaji kazi kwani iligawa fomu Septemba, 2013 na kujikuta zoezi la kupandisha walimu madaraja likifanywa kwa mikoa 12 ambayo nayo si kwa wilaya zote.
Mwananchi

No comments: