ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 24, 2014

AJALI MBAYA: MWANAFUNZI MAKONGO AFARIKI KATIKA AJALI YA BAJAJ NA LORI

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Makongo, Priscus Mallya, baada ya kufariki katika ajali ya lori na Bajaj.
Mwili wa Priscus Mallya ukiwa katikati ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi baada ya ajali.
Bajaji ambayo mwanafunzi alikuwa amepanda akielekea shuleni Makongo ikiwa eneo la ajali.

MWANAFUNZI wa kidato cha nne, Shule ya Sekondari Makongo, Priscus Mallya, amefariki dunia katika ajali iliyolihusisha lori na Bajaj katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi eneo la Bamaga, Dar.

Kwa mujibu wa watu waliokuwa eneo la tukio wakati ajali hiyo ikitokea, wamesema kuwa mwanafunzi huyo alikuwa ndani ya Bajaj pamoja na wenzake wawili wakielekea shuleni Makongo ambapo walikutana uso kwa uso na lori kisha kumrusha na kutokea upande wa pili marehemu.

(PICHA/STORI: ANDREW CARLOS, DENIS MTIMA/GPL)

2 comments:

Anonymous said...

Naipa pole familia.
Hii habari haijakamilika. Utafikiri imeandikwa na mtoto wa miaka 5. Hao wawili wengine waliokuwa na dereva wako wapi? Na wanaendeleaje? Kama hauna habari iliyokamilika kwanini wakimbilia kuandika nusu.

Nakushauri uchukue mafunzo mafupi ya habari wewe uliyeandika hii habari.

Anonymous said...

Rest is Peace and Please please please, This is so unfair! These bajajis should be more cearful. Too many accidents in Tanzania. This is slaughter!!!! My prayers to the family, Wow!!