ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 17, 2014

Boniface Makulilo azungumzia maisha katika jeshi la Marekani kwenye kipindi cha NJE-NDANI

Boniface Makulilo alipokuwa katika Jeshi la Maji la Marekani (Navy)
Mtanzania Boniface Makulilo ametumikia Jeshi la Maji (NAVY) hapa Marekani kwa miaka miwili na sasa ni mwanajeshi mstaafu (Veteran)
Amezungumza na Mubelwa Bandio wa Jamii Production kuhusu maisha yake ya jeshini na namna ambavyo watu toka nje ya nchi wanaweza kunufaika na mafao yaliyopo jeshini.
Ameeleza mengi ya manufaa ambayo wengi hatuyajui kuhusu maisha katika jeshi hilo.
Karibu uungane nasi
NJE-NDANI ni kipindi kutoka Jamii Production Washington DC kinachokujia moja kwa moja (LIVE) kila Jumamosi kuanzia saa 6 mpaka 8 mchana (saa za Marekani mashariki) ambacho kinaleta Habari na Taarifa kuhusu yale yanayotokea na kuwagusa waAfrika walio NJE na NDANI ya Afrika.

3 comments:

Anonymous said...

Haya nyie wanaume mnamuona kijana mwenzenu mwenye akili acheni ubishow wa kuuza sura kwenye FB wanaume wazima ata haya hamuoni ,kubedua midomo kwenye fb kama wanawake nyie ,kubadilisha nguo kama wanawake nyie ,kuvaa miwani mikubwa ya frame za mbao nyie na hapo makaratasi hamna hebu fateni nyayo za BOniface kashawamwagia mpunga .akili kichwani mwenu ,asante sana kaka boniface na bubelwa nimesikiliza clip yote na nimeipenda sana mbarikiwe kwa kweli .

Anonymous said...

Wewe kama umekosa cha kuongea bola ukae kimya labda mume wako ananuka kikwapa na unampenda kwa hivyo mimi napenda kuona mume wangu anapendeza jeshi sio kigezo kila mtu na anavyo taka kuwa kimaisha acha hiyo tabia mnaongea sana watanzania.

Anonymous said...

Wewe mdau wa pili acha hizo watanukaje watu vikwapwa wakati kuna deorant adi buy one get one free ,mkiambiwa ukweli mnaumia ,mtabaki na maisha ya kuangaika mpaka lini walati boniface ameshaeleza watu mnashida kibao na ma child support juu si bora tuu mjiunge na jeshi msaidie familia zenu na nyie wenyewe ,haya chechei basi .