ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 18, 2014

JUMUIYA YA WATANZANIA HOUSTON: TANGAZO LA MISA YA MSIBA

Mwanajumuiya mwenzetu Bw. Obedy Adam Mambya, amefiwa na baba yake mzazi, mzee Adam Mambya. Mzee Mambya amefariki wiki iliyopita tarehe 12 machi, 2014 huko Musoma-Mara Tanzania, baada ya kusumbuliwa kwa muda na sarakani (cancer) ya koo.
Napenda kuwataarifu kwamba kutakuwa na misa ya kumuombea marehemu, baba mpendwa wa Bw. Obedy Adam itakayofanyika Jumamosi ijayo(03/22/2014), muda ni saa kumi jioni(4pm). Wote mnakaribishwa na kwa niaba ya wafiwa natanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano wenu. Anuani ya ukumbi ni kama ifuatavyo:

9851 Meadowglen Lane, Houston TX 77042. Club House at Madison Park.
Kwa taarifa zaidi wasiliana na Shebby Pambweh: 832-858-5990
Obedy Adam: 832-563-3196
Asanteni,
Novastus Simba.

No comments: