ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 12, 2014

LICHA YA MIKOA YA KUSINI KUWA NA VIONGOZI WENYE NYADHIFA KUBWA SERIKALINI LAKINI SEHEMU HII ISIYO ZIDI UMBALI WA KM 70 IMEBAKIA KUWA KERO NA HISTORIA KUPITIKA KATIKA KIWANGO CHA LAMI LABDA YESU ASHUKE.

Msululu wa mabasi ya abiria na malori yakiwa hayajui hatma ya safari yao baada ya kukwama katika kijiji cha Sinza katikati ya Somanga - Nyamwage mkoani Lindi, kutokana na barabara wanayoitumia kupatwa na uharibifu mkubwa uliotokana na mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini.
Eneo hili lenye urefu wa kilometa 14,ndio eneo korofi sana kwenye barabara hii kuu itokayo Mtwara,Lindi mpaka Dar es Salaam.Picha na Mdau Paul Marenga,Lindi.




Katapila likifanya maarifa ya kufanikisha magari hayo kupita.
Msururu bado ni mkubwa sana.
Wasafiri wanaotumia magari yaliyokwama katika eneo hilo wakiwa wamesimama kuangania nini kinafanyika ili waweze endelea na safari yao.

2 comments:

Anonymous said...

Sijakuelewa mtoa mada, kwani kuna uhusiano gani kuwa na viongozi wengi wanaotoka kusini na ubovu wa barabara, je, unataka wafanyeje?upendeleo au.

Anonymous said...

Mtoa maoni namba moja, mada haizungumzii upendeleo. Nafikiri mtoa mada anataka viongozi kutoka kusini waongoze kama wale wenzao wa kaskazini ili barabara zao zifanane na zile zinazokwenda kaskazini. Mimi nadhani kama Yesu atafanikiwa kurudi, atakuta hayo magari yameshafika yakokwenda.