ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 19, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHITIMISHA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI KITAIFA WILAYANI MPWAMPWA MKOA WA DODOMA LEO.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtwisha ndoo ya maji Bi. Amina Rajab, mkazi wa Wilayani Mpwapwa, baada ya kuzindua rasmi Kisima cha Bomba la maji, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mradi wa Maji wa Wilaya ya Mpwapwa, Shadrack Matemba (wa pili kulia) wakati alipotembelea moja ya chanzo cha maji wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014. Kulia kwa Makamu ni Mama Asha Bilal na Waziri wa Maji , Profesa Jumanne Maghembe.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi Kisima cha Bomba la maji sikiliza wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo, Machi 19, 2014. Kushoto kwa Makamu ni Waziri wa Maji , Profesa Jumanne Maghembe,(kushoto) ni Mama Asha Bilal.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili ya kabila la Wagogo wakati alipokuwa akiwasili katika sherehe za maadhimisho ya Wiki ya Maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo.
 Baadhi ya wananchi wa Wilayani Mpwapwa wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akiwahutubia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya maji zilizofanyika Kitaifa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma leo.

3 comments:

Anonymous said...

wanakenua mimeno na kujifanya wanawajali sana walala hoi kumbe wanakuchekeni kama kweli kwa nini wao waku wote mafisadi wa ccm wasiwe wanaishi kama nyinyi maisha ya kawaida
ujinga mtupu

Anonymous said...

nishakushtukizia dj luke tukituma comment zetu kwa wasio wazanzibari huzi weki kwa walio wazanzibari unazitupa. no problem kazi njema mheshimiwa

Anonymous said...

ITS TRUE ANONYMOUS WA PILI NIMEJARIBU KUTUMA COMMENT KWA WABARA WENZAKE HUYU LUKE ANAZITUPA TU KWA WAZANZIBARI UKIWASEMA TU YUKO MBIONI KUZIWEKA SYSTEM AT WORK