Chama cha Madaktari wa Tanganyika (MAT), kimeonya kuwa Tanzania
kutoruhusu mapenzi ya jinsia moja kwani taifa haliwezi kumudu madhara
yatokanayo na matendo hayo.
Alisema ushoga husambaza Virusi Vya UKIMWI (VVU) kwa kasi na homa ya ini ambayo inaua kwa haraka kuliko UKIMWI na kuitahadharisha nchi kutojiingiza kwenye ndoa hizo ambazo husababisha matatizo makubwa kiafya.
Alihoji iweje nchi zilizoendelea zinazoelewa kuwa kujamiiana kinyume cha maumbile kunasambaza maradhi kwa kasi kuyalazimisha mataifa maskini kutambua ngono hizo zenye madhara mengi?
“Umaskini uliopo unalifanya taifa lisimudu kutibu malaria ya kawaida au kipindupindu sembuse kuruhusu ngono za kinyume cha maumbile zinazosambaza magonjwa mengi kuanzia UKIMWI, homa ya ini na maradhi yatokanayo na ngono - kisonono na kaswende.”Msimamo huo ulitolewa na Rais wa MAT, Dk. Primus Saidia, alipozungumza na NIPASHE Jumapili, kuhusu kitisho cha mataifa ya Magharibi kuilazimisha Afrika kutambua ndoa za jinsia moja.
Alisema ushoga husambaza Virusi Vya UKIMWI (VVU) kwa kasi na homa ya ini ambayo inaua kwa haraka kuliko UKIMWI na kuitahadharisha nchi kutojiingiza kwenye ndoa hizo ambazo husababisha matatizo makubwa kiafya.
Alihoji iweje nchi zilizoendelea zinazoelewa kuwa kujamiiana kinyume cha maumbile kunasambaza maradhi kwa kasi kuyalazimisha mataifa maskini kutambua ngono hizo zenye madhara mengi?
“Maradhi ya ngono huambukizwa kiurahisi kwa kujamiiana kinyume cha maumbile. Hii ni kwa sababu njia hii haikuandaliwa kwa ajili hiyo,”
alisema Dk. Saidia.
Alifafanua kuwa sababu ya kueneza maradhi ni kwamba sehemu za siri za wanawake zimeandaliwa kujamiana na njia yao ina vilainishi kwa ajili ya tendo hilo, tofauti na njia ya haja kubwa ambayo haikuandaliwa kwa ajili ya ngono.
Akizungumzia kusambaa VVU kwa kasi alisema kuwapo uchafu mwingi na vimelea vya magonjwa kwenye njia ya haja kubwa maumbile yameweka tezi kinga (CD) nyingi ili kuupusha mwili na magonjwa yanayoweza kuletwa na vimelea vilivyoko kwenye choo.
Hata hivyo VVU vinashambulia CD na kuingiza virusi mwilini kwa urahisi wakati wa kujamiana kinyume cha maumbile.

“Mataifa yaliyoendelea yamejiandaa na yanaweza kutatua matatizo hayo, wana chanjo za homa ya ini, zipo dawa za kufubaza makali ya VVU lakini si Afrika wala Tanzania yenye uwezo huo,”
alionya Rais wa MAT.
Alitaja kifua kikuu, malaria, homa za watoto na kuondoa umaskini kuwa yanayohitaji kipaumbele na si ushoga.
Dk. Saidia alipinga madai kuwa ushoga ni hali ya kuzaliwa bali alisema ni tabia za kujifunza.
Imeandikwa na GAUDENSIA MNGUMI, NIPASHE JUMAPILI

3 comments:
Ameen doctor maneno yako sadakta.
Daktari Wamesema: Bado infrastructure yetu haiko tayari kwa hayo mambo.
DUNIA YA TATU TUNAIGA MAMBO AMBAYO YANALETWA KUSUDI TUPATE MAGONJWA WATUUZIE MADAWA YAO WANAYOTENGENEZA, TUFUMBUE MCHO,TUSICHUKUE KILA WASEMALO.
Mama golden
Post a Comment