Mapadri Batolomeo Bazemo (kushoto) na Padri Jean Marie wakiongoza ibada ya misa ya kiswahili ya kumuombea marehemu Dr. Fulgence Kazaura iliyofanyika katika kanisa la Mt. Camillus la Silver Spring, Maryland. Mapadri wote waliongoza Ibada kwa lugha ya kiswahili. Padri Batolomeo Bazemo anatokea Ivory Coast, lakini ni raia wa Burkina Fasso na alishafanyakazi ya Mungu na aliishi Manzese, Dar es Salaam, Tanzania miaka ya nyuma. Padri Jean Marie yeye ni raia wa DRC.
Mtoto wa marehemu Sima Kazaura (kulia), akiwa pamoja na Aunty yake Leticia kwenye Ibada ya Misa ya kumuombea marehemu Dr. Fulgence Kazaura iliyofanyika Jumaosi March 1, 2014 katika kanisa la Mt. Camillus.
Kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula akifuatilia Ibada ya misa ya kumuombea marehemu Dr. Flugence Kazaura iliyofanyika katika kanisa la Mt. Camillus Silver Spring, Maryland.
Mmoja ya wanafamilia akisoma neno
Sunday Shomari akiongoza matangazo kanisani hapo.
Oliver Gervas akisoma wasifu wa marehemu.
Aunty Leticia akielezea jinsi alivyomfahamu marehemu.
Balozi Liberata Mulamula akitoa pole kwa wafiwa pia alimuelezea jinsi alivyomfahamu marehemu na kuelezea jinsi alivyomfahamu marehemu na msiba ulivyomgusa kwani mdogo wake wa mwisho Edwin ameoa mtoto wa kwanza wa marehemu aliyemtaja kwa jina moja la Koku.
Juu na chini ni Picha ya pamoja
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
2 comments:
SIMA POLE SANA JAMANI SIJAJUA KAMA UMEFIWA MPAKA NIMESOMA HUMU KATIKA BLOG YA VIJIMAMBO POLE SANA MUNGU AKUPE MOYO WA KUSTAHAMILI,POLE SANA AMETUTANGULIA NA SISI TUPO NJIANI MUNG AMLAZE MAHALI PEMA MZAZI WAKO AMEN.
MT.VERNON,
sima pole sana na ndugu na jamaa na marafiki wote wa wana familia poleni sana jamani mungu akubarikini daima na akupeni moyo wa kustahamili katika kipindi hichi cha msiba poleni sana jamani.
nitakutafuta sima pole sana jamani.
mt.vernono
Post a Comment