Advertisements

Saturday, April 19, 2014

Dk. Salim kushuhudia Usiku wa Mwambao Asilia Jumamosi hii April 19


Na Andrew Chale
KATIBU Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa ya Afrika (OAU, sasa Umoja wa Afrika - AU), Dk. Salim Ahmed Salim, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika onesho maalum la Usiku wa Mwambao asilia utakaosindikizwa na bendi za Dar Modern Taarab na Nadd Ikhwan (Malindi), ndani ya ukumbi wa Travertine, Magomeni jijini Dar es Salaam,Jumamosi hii April 19

Mlezi wa heshima wa kundi la Dar Modern Taarab, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, alisema Dk. Salim ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, amethibitisha kujumuika na wadau na mashabiki wa taarabu asilia.
Idarous alisema wadau wa muziki wa taarabu watafurahia usiku huo wa Mwambao Asilia kutoka kwa wanamuziki nguli wa miondoko hiyo Bara na Visiwani.
“Usiku wa Mwambao Asilia, utasheheni magwiji wakongwe wa muziki wa taarabu nchini, kutoka kundi la Dar Modern Taarab na Nadd Ikhwan, ambao wataporomosha nyimbo za taarabu asili za zamani na za sasa,” alisema Idarous.
Aliongeza kuwa pia usiku huo utapambwa na ‘surprise’, ikiwemo watu mbalimbali kupita kwenye zulia jekundu ‘red carpet’ na kupiga picha za ukumbusho na mastaa watakaohudhuria.
Alisema katika usiku huo, kiingilio kitakuwa ni sh 10,000 ambapo tayari tiketi zilishaanza kuuzwa sehemu mbalimbali.
Idarous alizitaja sehemu hizo kuwa ni duka la Fabak Fashions, Regency Park Hotel Mikocheni na Dar Modern Taarab Hall Magomeni Ifunda.
Onyesho hilo pia limedhaminiwa na Times FM, Fabak Fashions na www.nakshi255.com

No comments: