Advertisements

Tuesday, April 15, 2014

Gurumo alivyotabiri kifo chake

Gurumo. 
Kwa mujibu wa binti wa mwanamuziki huyo Mariamu Gurumo, Jumatano wiki iliyopita alikwenda kwa baba yake na kumuaga kuwa wanataka kwenda Kisarawe yeye na ndugu zake wawili yaani Omari na Mwazani, Hata hivyo baada ya kumwambia hivyo, Gurumo aliwaambia kwamba anataka kuungana nao katika safari hiyo.

MWANAMUZIKI mkongwe, Muhidin Gurumo, 73 aliyefariki dunia juzi Jumapili ni kama alikitabiri kifo chake baada ya kutembelea na kufanya usafi katika makaburi ya nyumbani kwao.
Kwa mujibu wa binti wa mwanamuziki huyo Mariamu Gurumo, Jumatano wiki iliyopita alikwenda kwa baba yake na kumuaga kuwa wanataka kwenda Kisarawe yeye na ndugu zake wawili yaani Omari na Mwazani, Hata hivyo baada ya kumwambia hivyo, Gurumo aliwaambia kwamba anataka kuungana nao katika safari hiyo.
“Hatukuwa na mpango wa kwenda na baba lakini aling’ang’ania kwa madai kuwa hatuwezi kwenda bila yeye, na siku ya safari alituamsha asubuhi, alifurahi sana sijui kwa nini,”alisema .
Kwa mujibu wa Mariamu, kabla ya kufika Masaki walipita Kibuta, na kuangalia makaburi na kusoma dua na walipofika Masaki walifanya hivyo hivyo kwenye makaburi ya huko ambayo yapo vilimani na mvua ilikuwa inanyesha lakini baba yao aliwaambia wafanye hivyo pamoja na mvua.
“Baada ya kufagia makaburi hayo tuliloa, baada ya hapo alinunua dafu na kunywa maji yeye, mimi, Mwazani na Omari, sikufahamu kwanini alifanya hivyo, lakini alikuwa na furaha nilijua na furaha yake tu, kumbe alikuwa anatuaga,”alisema.Akieleezea hali ilivyokuwa hadi baba yake anafikwa na umauti, Mariamu alisema saa moja asubuhi siku iliyofuata baba yake alimpigia simu na kumtaka awajulie hali ndugu zake na baada ya kuambiwa wazima alimwambia yeye anaumwa. “Nilipomwambia utapona, aling’ang’ania anaumwa, alirudia mara mbilimbili hadi akanishitua, ingawa niliendelea na shughuli zangu,” alisema.
Mariamu anabainisha kuwa saa saba za usiku alipigiwa simu na kuambiwa hali ya baba yake ni mbaya sana, walimpeleka hospitali ya Muhimbili huku akipumua mwili mzima na kulalamika anaumwa.
“Ilikuwa ni Jumamosi na hospitali hakukuwa na madaktari, manesi waliokuwapo walikuwa wachache, wakasema anatakiwa achukuliwe damu, akapewa kitanda,’’ alisema.
“Jumapili alikuwa anajisikia vibaya sana, na alikuwa anatapatapa hadi akakata roho,’’ alisema.
Mazishi ya Gurumo yanatarajia kufanyika leo Jumanne, kijijini kwao Masaki, Kisarawe Mkoa wa Pwani.
Gredit:Mwanaspoti

No comments: