ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, April 27, 2014

HIVI NDIVYO SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANZANIA ZILIVYOFANA WAHSINGTON DC,WATANZANIA WAFURIKA

Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Watanzania hapa Washington DC kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano.Mh:Mwigulu Nchemba akiongozwa na Balozi wa Tanzania hapa Washington DC Bi.Libereta Mulamula Kuelekea Kufungua Sherehe za Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania hapa Washington DC.Mke wa Mh:Mwigulu Nchemba (Kulia)akisalimiana na Mwanamitindo Maarufu wa Mavazi hapa Washington DC na Viunga Vyake Miss Temeke wa "KWETU FASHION".

Ukuta Umependeza kwa Baongo Kubwa la Miaka 50 ya Muungano hapa Ubalozini Washington.Mh:Mwigulu Nchemba akitembelea Mabanda ya Maonesho ya Vitu Mbalimbali vya asili ya Tanzania nje ya Jengo la Ubalozi wa Tanzania hapa Wahsington DC.
Mh:Mwigulu Nchemba akipata maelezo kuhusu Vitenge na Khanga zinazouzwa Nje ya Jengo la Ubalozi wa Tanzania zenye Kutengenezwa Tanzania.
Maonesho yanaendelea hapa Washington DC,Ubalozi wa Tanzania.Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano yamefana sana Washington DC.
 Mh:Mwigulu Nchemba akikata Utepe Kuashiria Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano hapa Washington Dc Zimefunguliwa rasmi,Kulia Kwake ni Balozi Libereta Mulamula na Kulia Kwake ni Waziri anayeshughulikia Muungano-Zanzibar Mh:Mwinyihaji Makame.

Ubunifu:Miaka 50 Ya Muungano wa Tanzania hapa Washington DC.Viongozi wakionja Chakula cha Asili cha
Tanzania kilichopikwa hapa Washington DC,Ugali wa Mihogo,Makande,Ndizi,Kisamvu n.k Vilikuwepo.Katikati ni Bwana Okoka Sanga akiwa na Viongozi wa Kitaifa waliofika Kuadhimisha Miaka 50 ya Muungano hapa Washington,Okoka Sanga ni Mtengenezaji Maarufu wa Kadi na Mifuko ya Zawadi hapa Washington DCMaadhimisho yanaendelea huku Kuta za Jengo la Ubalozi zikiwa Zimepambwa Picha za Viongozi wetu wa Kitaifa.
Bidhaa za Bakharesa pia Zilikuwepo kwenye Sherehe hizi za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano,Hakika Zimefana sana.
Tanzania Nchi inayopendwa na Mataifa Yote Duniani,Kisiwa cha Amani na Upendo.

I love Tanzania,Bibi huyu wa Kizungu alipata Kuishi Tanzania na Kufanikiwa Kupandisha Sehemu ya Mlima Kilimanjaro,Hapa anahamasisha Watu Kupanda Mlima Kilimanjar.
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Kutoka Huston-Texas Waliofika hapa Washington DC Wakiwa katika Picha ya pamoja na Mh:Mwigulu Nchemba mara baada ya Kuzungumza Machache kuhusu Kuimarisha Chama hapa Marekani,
Mh:Mwigulu Nchemba akimvisha Skafu ya Tanzania huyu Mtoto wa Kizulu-South Africa aliyepiga Ngoma na kufanya Umati Kushangilia kwa Shangwe,Baba yake wa huyu Mtoto aliwahi Kuishi Tanzania Mwaka 1982.
 Kikundi cha Wacheza Ngoma ya Asili cha Watanzani waishio hapa Marekani Wakitumbuiza Kwenye Sherehe za Miaka 50 ya Muungano.
Mh:Mwigulu Nchemba akibadilishana Mawazo na Watanzania nje ya Jengo la Ubalozi hapa Washington DC.Kwetu FashionNje ya Jengo la Ubalozi Watanzania wanabadilishana Mawazo,Wamepata Fursa yakuwa pamoja kwa sababu ya Muungano Wetu uliofikisha Miaka 50 hii leo.Mtanzania akiwaongoza wazungu hawa Kula chakula cha Asili cha Tanzania. Miss Tanzania wa hapa Marekani aliyeshinda Mwaka Jana 2013/2014 akiwasili Ubalozini tayari kwa Kuungana na Watanzania Kusherekea Miaka 50 ya Muungano.Tanzani Is All AaboutUkodak Unahusika.
 Watanzania Wamefurahi sana Hapa Washington DC kuadhimisha Miaka 50 ya Muungano,Wamejitokeza Kwa Wingi sana,Hivi ndivyo Muungano Ulivyofana Miaka 50,Nyama Choma na Vyakula vya asili vimepatikana Kwa Wingi hapa TANZANIA HOUS Washington DC.Tanzania Culture is All about.
Maadhimisho yamefana sana,Mtoto akionesha Uwezo wa Kucheza Ngoma ya Asili.Chombo cha Habari "SAUTI YA AMERIKA'VOA nao Walijumuika na Watanzania hapa Marekani,.Mtangazaji Hamza Mwamoyo akiwana Viongozi wa Serikali ya Tanzania Mh:Mwigulu NChemba (Kulia) na Mh:Mwinyihaji(Kushoto) baada ya Kufanya Kipindi kitakacho rushwa Voice Of America.
Balozi Mulamula akimkaribisha Askari wa Jeshi Kutoka Ubalozi wa Nigeria hapa Washington DC.Col.Mutta Kulia wa Ubaliozi wa Tanzania akimkaribisha Kiongozi Kutoka Ubalozi wa Camerron hapa Washington DC.Mapokezi yanaendelea kwa Wageni Kutoka Mataifa Mbalimbali waliofika Kuhudhuria Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania hapa Washington DC.
 Askari wa Mataifa Mbalimbali waliojumuika na Watanzania Kusherekea Miaka 50 ya Muungano Kutoka Kushoto ni Nigeria,Poland,Zimbabwe na Zambia waki kwenye Picha ya pamoja na Mh:Mwigulu NchembaKushoto ni Ndugu Mrisho Mzese Kutoka Maryland na Ndiye Mwenyekiti wa Shina la CCM  Maryland.Mh:Mwigulu Nchemba akiendelea Kusalimiana na Watanzania Mbalimbali walofika kwenye Ukumbio wa Marriott Hotel hapa Washington DC kusherekea Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.
Mh:Mwigulu Nchemba akisalimiana na Askari wa Jeshi kutoka Ubalozi wa Nigeria aliyefika Kujumuika na Watanzania kwenye Sherehe za Muungano wa Miaka 50 wa Jamhuri ya Muungano Ya Tanzania.Watanzania wakiwa Kwnye Mavazi ya Kiafrica zaidi
Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 zimefana sana hapa Washington DC.Tanzania ianapendwa sana na Mataifa Mengine ya Africa,Kushoto ni Raia wa Nigeria na Kulia ni Raia wa Cameroon wamefika Kuungana na Watanzania hapa Washington DC kusherekea Miaka 50 ya Muungano.
 Mh:Mwigulu Nchemba akibadilishana Mawazo na hawa Wazungu waliopata Kuishi Nchini Tanzania miaka ya 1990's.
Tanzania Is All about kwa hapa Washington DC,Tuudumishe Muungano Wetu.Huyu Dada wa Kitanzania amesafiri Kutoka Calfoni hadi Washington Kwaajili ya Kuuongoza Watanzania kuimba Wimbo wa Taifa wa Tanzania na Marekani,Ameonesha Kipaji chake cha ajabu cha Kuimba Nyimbo zote mbili kwa Ustadi Mkubwa sana.

Balozi Libereta Mulamula akiwa na Mme wake alipomuita Kwaajili ya Kumtambulisha kwa Watanzania waliofika kusherekea Miaka 50 ya Muungano.
Viongozi wakisikiliza Kwa Makini maneno ya Balozi Mulamula(hayupo Pichani).
 Mmoja ya Viongozi wa Serikali ya Marekani akifurahia Umoja na Urafiki wa Tanzania na Marekani kidiplomasia,Na ameomba uendelee Kudumishwa.
Hapa akitosi Glasi na Balozi Mulamula Kuonesha Upendo na Mshikamano Miongoni Mwa Watanzania na Serikali ya Marekani.
Mh:Mwinyohaji Makame akizungumza n Watanzia hapa Washington DC kuhusu Umuhimu wa Muungano Kwa Wananchi wa Zanzibar,Amesisitiza Watanzania Wajikite kujadili maswala ya Maendeleo na sio Kuongeza Idadi ya Serikali kitu ambacho kinapoteza Muda na hakina Manufaa kwa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa Ujumla.Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza n Watanzania na Wananchi wa Mataifa Mbalimbali waliofika Kusherekea Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania,Mh:Mwigulu amesema ni Wajibu kwa Kila Mmoja wetu katika Kizazi hiki kuandika historia ya kipekee kwa Kuulinda na Kuudumisha Muungano wetu kwa Miaka 50 zaidi,Kizazi kijacho kitawahukumu Watanzania endapo Muungano Utavunjika kwa Sababu tu ya Kupenda Vyeo na Ukosefu wa Utashi wa Kisiasa.
 Watanzania hawa Wakipata UKODAK kwenye sherehe za Muungano hapa Washington DC.

Nafasi ya Kupata Ukodak na Mh:Mwigulu na Mke wake(Kushoto).Viongozi wa Chama Cha mapinduzi Kutokea TEXAS.
Mh:Mwigulu Nchemba akiingia na Mh:Balozi Libereta Mulamula kwenye Usiku wa Muungano hapa Washington DC.
 Mc akiendesha Shughuli kwenye USiku wa Miaka 50 ya Muungano.
Usiku wa Muungano Umefana sana,Watanzania wapo Wamoja.Tutaulinda Muungano Wetu.
 Watanzania Wanaipenda Tanzania yao.
Viongozi wa Mataifa Mbalimbali katika Picha ya Pamoja na Balozi Libereta Mulamula,Mh:Mwigulu Nchemba na Mh:Mwinyihaji Mara baada ya Mh:Mwigulu NChemba kumaliza Kuzungumza na Watananzania.Safu ya Viongozi wa Jumuia za Watanzania kwenye Majimbo mbalimbali hapa Marekani wakiwa katika Meza ya pamoja na Mh:Balozi Mulamula na Mh:Mwigulu Nchemwa wakati wa Usiku wa Muungano hapa Washington DC.Sehemu ya Umati wa Watanzania waliofika Kwenye Usiku wa Muungano hapa Washington DC.
Usiku wa Muungano Ulipambwa na Nyimbo za Kitanzania tu,Hapa Mziki unaendelea Kusherekea Miaka 50 ya Muungano Wa Tanzania.
Mh:Mwigulu Nchemba akizunguma na Watanzania Kwenye Usiku wa Miaka 50 ya Muungano hapa Washington DC.Mwigulu amezungumzia Kuhusu Uraia Pacha na Kuwaahidi Watanzania Kuungana nao Kuipata haki hiyo Kikatiba na Chama cha Mapinduzi kimependekeza hilo kwenye Rasimu ya Katiba Mpya,Pia amezungumzia Sababu za Kiuchumi kuhusu Mzigo wa Serikali ya tatu inayopendekezwa na Rasimu huku akiwapa Uhuru Wataanzania Kutafakari kwa Kina kuhusu Jambo hilo,na Mwisho amezungumzia kuhudu dhamira ya Wazi ya UKAWA kuvuruga Mchakato wa Katiba,na dhamira hiyo imepangwa kutoa awali wakati wa Ukusanyaji wa Maoni na hata Kwenye Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la katiba.Hivyo Kususia kwao Bunge ni jambo walilopanga na Wamelitekeleza.Mh:Mwigulu amepeleka pongezi kwa Watanzania Wote kwa Kupuuzia Kitendo hicho walichokifanya UKAWA kwsababu hakikuwa cha Kizalendo na Kimelenda Kuligawa Taifa.
 Picha/Maelezo na Sanga Festo-Washington DC
26/04/2014

4 comments:

Anonymous said...

Swali la kizushi, hivi ni Watanganyika tuuu wanasheherekea huu Muungano?? Mbona Zanzibar hawako saana kihivyo kwenye kusherehekea?? Umeshawahi jiuliza hilo swali??

Anonymous said...

Huo ubunifu uliofanywa wa watermelon kunadikwa "50th Tanganyika & Unguja" sijui kimakosa au umekusudiwa au kutofahamu. Vipi Pemba haimo ktk muungano ? Ingekuwa imeandikwa Tanganyika & Zanzibar tungekuelewa.

Anonymous said...

pemba haimo wapemba nani anawajua ndo maana wanafanikiwa wakiwa peke yao na kufanya yao

Anonymous said...

mzanzibari halisi mwenye uchungu na nchi yake haji hapo katika viparty party vyenu mzanzibari anayejitambua na kuwa na uchungu wa nchi yake na kutaka mamlaka kamili ya nchi yake haji hapo kishaamka kishagutuka kishashtuka hajalala tena usingizi wa ponooo na hana maskhara na utumbo utumbo huu ndo maana humuoni mzanzibari halisi

lakini mzanzibari wa kuchovyaa aliye changanya na asiyejijua huku yupo na huku yupo ndo wamo tele humuuu

hongereni wazanzibari halisi msiokwenda katika party hii inshallah Allah akubarikini sana na ishallah mtakuja kupata nchi yenu very soon inshallah Allah ma amin