Advertisements

Thursday, April 24, 2014

HOMA YAPANDA MTANANGE WA KIMANJARO STARS NA ZANZIBAR HEROES

WAZANZIBARI KUTOKA MAJIMBO YA JIRANI KUINGIA DC JUMAMOSI.
KUIONGEZEA NGUVU ZANZIBAR HEROES, 
WAAGIZA JEZI TOKA ZANZIBAR
JEZI KUINGIA DC IJUMAA
Timu ya Boston inayoundwa na asilimia kubwa ya Wazanzibari.

Kiwewe cha mechi ya Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes imeanza kupanda baada ya habari nyeti kutoka chanzo cha kuaminika ambazo Vijimambo imezipata ni kwamba Wazanzibari kutoka Masachusetts, New Jersey na New York wakiwemo watoto watatu wa Mhe. Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi  wataungana na wenzao wa DMV kwenye mechi kali ya kusherehekea maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano itakayofanyika siku ya Jumapili April 27, 2014 Creencastle, Silver Spring, Maryland na Mhe. Balozi Liberata Mulamula kuwa mgeni rasmi.

Wachezaji wote DMV wanaendelea na mazoezi makali katika viwanja wa Meadowbrook Park na Ijumaa April 25, 2014 kutakuwepo na mazoezi ya mwisho mwisho ya kujiandaa na mtanange huo unaosubiliwa kwa mbwembwe nyingi na mashabiki wa kabumbu wa DMV na majimbo ya jirani.

Wazanzibari wamesikika wakitamba kuibuka na ushindi mnono kwenye mechi hiyo ambayo imekua gumzo kila kona unayopita wachezaji na mashabiki wakitambiana na kila mmoja akidai kuibuka na ushindi.


No comments: