Advertisements

Friday, April 25, 2014

KINANA AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MSUMBIJI JIJINI DAR ES SALAAM


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Msumbiji  Dk.Alberto Clementino Antonio Vaquina ,makao makuu ya chama Ofisi Ndogo Lumumba ,Katika ugeni huo Waziri Mkuu wa Msumbiji aliongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Msumbiji Dr.Eduardo Baciao Koloma,Bslozi wa Jamhuri ya Msumbiji Dr.Vicente Mebunia Veloso na Mshauri wa Waziri Mkuu katika Masuala ya Kidiplomasia Mr.Tarcisio Baltazar Buanahagi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi kutoka kwa  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Msumbiji  Dk.Alberto Clementino Antonio Vaquina mara baada ya kumaliza mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Chama Lumumba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Msumbiji  Dk.Alberto Clementino Antonio Vaquina mara baada ya kumaliza mazungumzo kwenye ofisi ndogo za CCM Lumumba.

No comments: