Advertisements

Friday, April 18, 2014

MAMA AMSAMEHE NA KUMFUNGUA KITANZI MFUNGWA ALIYE HUKUMIWA KUFA KWA KUMUUA MWANAE


Wanasema uchungu wa mwana aujuae mzazi! Na kutokana na uchungu huo wa mama, ni vigumu kumshawishi akae meza moja na mtu aliyemuua mwanae kwa makusudi tena kwa kumpiga hadi kuhakikisha anakata roho.

Lakini imekuwa tofauti na jambo lililowaacha mdomo wazi umati wa watu uliohudhuria kushuhudia kunyongwa kwa mwanaume aliyemuua kijana mwenye umri wa miaka 18 nchini Iran ambako hukumu ya kunyongwa hadharani ni kawaida kwa mtu aliyepatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia, pale ambapo mama mzazi wa marehemu alipoingilia na kumfungua kitanzi muuaji huyo sekunde ya mwisho.


Kwa mujibu wa The Guardian, mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Balal alikuwa tayari amefungwa kitambaa cheusi na kuvalishwa kitanzi akisubiri amri ya kitanzi kufyatuliwa, ghafla mama huyo alimzaba kibao usoni na kuanza kumfungua kitanzi akisaidiana na mumewe!

“Mimi ni mtu wa imani.” Alisema mama huyo aliyefahamika kwa jina la Samereh Alinejad. “Nilipata ndoto ambayo mwanangu alikuwa ananiambia kuwa yuko katika sehemu nzuri na yenye amani…baada ya hapo, ndugu zangu wote, hata mama yangu, wakaanza kunihimiza nimsamehe muuaji huyu.”

Balal alihukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga vibaya Abdollah Hosseinzadeh (18) hadi kumuua katika ugomvi uliotokea mtaani kati yao mwaka 2007.

2 comments:

Anonymous said...

Subhanallah

Anonymous said...

God Bless you heart Mama